Thursday, April 20, 2023

UCSAF KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI-MHANDISI KUNDO


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali kupitia UCSAF imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano nchi nzima.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Mhandisi Kundo Mathew Wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Mhe Jonas William Mbunda aliyetaka kufahamu lini Serikali itajenga Minara ya simu katika Kata za Kikolo, Mbangamao, Kitanda na Kagugu – Mbinga.

Mhe Kundo amesema kuwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, UCSAF imeainisha kata ya Kitanda hususani kijiji cha Lupilo na Mlembeni katika zabuni iliyotangazwa mnamo tarehe 24 Oktoba, 2022 na kufunguliwa tarehe 31 Januari, 2023.

Mhe Kundo amesema kuwa zabuni hiyo utekelezaji wake umeanza na unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2023/2024. 

Amesema kuwa katika upande wa kata zilizowasilishwa kuwa na changamoto za mawasiliano, Kata za Kikolo, Mbangamao, na Kagugu, UCSAF itakwenda kufanya tathmini katika maeneo yayoliwasilishwa ili kubaini changamoto halisi zilizopo. 

Aidha, Endapo utatuzi wa changamoto zitakazobainika utahitaji ujenzi wa minara mipya, kata hizo zitaainishwa na kuingizwa kwenye zabuni itakayotangazwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.

MWISHO

No comments:

Post a Comment