Wednesday, April 19, 2023

SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU


Na Saida Issa, Dodoma

Mbunge wa kilwa kusini Ally Kassinge ameiomba Serikali kupitia TAMISEMI kuhakikisha inaendelea kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu hasa kumaliza changamoto za madawati.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma amesema kuwa Serikali imejitahidi kuboresha sekta ya elimu hasa kwa kujenga Madarasa pamoja na nyumba za walimu lakini madawati bado ni changamoto.

"Serikali ya Dkt.Samia imeendelea kuhakikisha sekta ya elimu inazidi kuimarika lakini changamoto bado ipo katika madawati kupitia bajeti ya TAMISEMI napenda kuishauri Serikali kuendelea kukabilia na changamoto kama upunguvu wa madawati katika shule ambazo zinajengwa,"amesema.

Amesema kuwa wabunge wamekusudia kuipitisha bajeti ya TAMISEMI kwani ndio bajeti ambayo inabeba bajeti za halmashauri zote na zinagusa kila jimbo.

No comments:

Post a Comment