Thursday, July 8, 2021

WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA BALOZI WA ISRAEL//AMUHAKIKISHIA KUENDELEZA USHIRIKIANO SEKTA YA KILIMO

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo leo tarehe 8 Julai 2021 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw Eyatan Hatzor na wawakilishi wa Taasisi ya CultiviAid Dkt Tomer Malchi pamoja na Bw. David Zukerman wa nchini Israel. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw Eyatan Hatzor akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda  Jijini Dodoma leo tarehe 8 Julai 2021. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo, wawakilishi wa Taasisi ya CultiviAid Dkt Tomer Malchi pamoja na Bw. David Zukerman wa nchini Israel. 
Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw Eyatan Hatzor na wawakilishi wa Taasisi ya CultiviAid Dkt Tomer Malchi pamoja na Bw. David Zukerman wa nchini Israel wakimsikiliza kwa makini mwenyeji wao Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda wakati wakifanya mazungumzo kuhusu kuendeleza sekta ya kilimo, Leo tarehe 8 Julai 2021 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo ya Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda na Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw Eyatan Hatzor na wawakilishi wa Taasisi ya CultiviAid Dkt Tomer Malchi pamoja na Bw. David Zukerman wa nchini Israel. Leo tarehe 8 Julai 2021 Jijini Dodoma.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw Eyatan Hatzor na wawakilishi wa Taasisi ya CultiviAid Dkt Tomer Malchi pamoja na Bw. David Zukerman wa nchini Israel.


Katika mazungumzo hayo yaliyotanguliwa na mazungumzo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo yalijikita katika kuimarisha mashirikiano baina ya Tanzania na nchi ya Israel katika kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini.


Katika majadiliano hayo mambo mengi yameibuliwa ambayo ni pamoja na Kuimarisha eneo la umwagiliaji katika zao la zabibu na maeneo mengine katika mazao mbalimbali ya kilimo hapa nchini. 


Katika Mazungumzo hayo Waziri wa kilimo Prof Mkenda amewahakikishia kuwa serikali ya Tanzania ipo tayari na itatoa ushirikiano katika kuimarisha mashirikiano na Israel ili iweze kunufaika na teknolojia ya Kilimo ya nchini Israel.


Waziri Mkenda amewajulisha kuwa Wizara ya Kilimo imedhamiria kuendesha kilimo cha kizimba kwa ajili ya ajira za vijana na kukuza kipato kupitia kilimo cha pamoja ambacho kwa upande wa ujuzi Wizara inashirikiana pamoja na SUGECO kuweza kufikia lengo la vijana kushiriki kikamilifu katika kilimo cha Kizimba kwa kushirikisha pia vijana wanaorejea toka mafunzoni Israel.


Waziri Mkenda amesisitiza kuwa programu hiyo ni nzuri ila inahitaji ifanyiwe maboresho kwenye sifa za wadahiliwa kwani imelenga tu kwa wanafunzi waliopo vyuoni lakini inabidi iangalie namna bora ya kudahili watumishi hasa maafisa ugani ili waweze kuongezewa uwezo kupitia mafunzo hayo.


Prof Mkenda amesema kuwa kupitia mashirikiano hayo Wizara ya kilimo itatumia fursa hiyo kuwaongezea ujuzi maafisa ugani kupitia wataalam wa nchini Israel.


Naye Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel nchini Bw. Eyatan Hatzor amebainisha kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya uzalishaji kwa kuwa na hali ya hewa nzuri na kuwa na upatikanaji wa maji wa uhakika ambapo amesema fursa hiyo haijatumika kikamilifu katika kuongeza tija na uzalishaji.


Kuhusu Uendelezwaji wa progamu ya vijana wa kitanzania anaomaliza mafunzo ya miezi kumi na moja nchini Israel, Bw Eyatan Hatzor meshauri kuanzishwa maeneo ambayo yatawakusanya vijana sehemu moja na kuweza kufanya kilimo cha pamoja (Block Farming) ili waweze kutoa elimu waliyoipata nchini Israel katika kuendeleza teknolojia mbalimbali walizojifunza wakiwa Israel na kuzitumia hapa nchini.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo amesema kuwa nchi ina uhaba wa maafisa ugani wenye weledi katika zao la zabibu na hivyo kupelekea uzalishaji wa zabibu kuwa wenye tija ndogo sana ukilinganisha na fursa kubwa iliyopo nchini hivyo ushirikiano huo utakuwa chachu ya kuimarisha maafisa ugani nchini.


MWISHO

No comments:

Post a Comment