Thursday, July 8, 2021

MBUNGE WA LINDI MJINI AWAFUNDA VIJANA KUWA WABUNIFU

 




Mbunge wa Lindi Mjini Hamida Abdallah akifungua baraza la Vijana la Manispaa ya Lindi huku akiwasihi kuwa na Ushirikiano na upendo katika kuhakikisha kila kijana anakuwa na ubunifu wa hali na mali katika kuhakikisha anajishughulisha kufanya kazi na sio kukaa tu.


Akizungumza katika baraza hilo la Vijana Mhe Hamida amewasii Vijana kuendelea kujiunga na Veta ambayo Serikali inangalia jicho la kipekee katika kuwapa Mafunzo Mbalimbali.


"Nawapenda sana Vijana wangu wa Manispaa ya lindi niwaombe Mfanye kazi kwa juhudi zote na mnajua Rais Mama Samia Suluhu Hassan anawapenda Sana Vijana na ndio maana hata katika uongozi mbalimbali katika Taifa letu Vijana mnaongoza kuwekwa katika nyadhifa mbalimbali"


Mwisho.

No comments:

Post a Comment