Monday, December 7, 2020

Waziri Mteule wa Viwanda na Biashara Mhe Mwambe atembelea Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania Jijini Dar es salaam

Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe Goodfrey Mwambe (Katikati) akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa afisa wa kiwanda cha Kahawa (Mbinga Coffee) wakati alipotembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 -9 Desemba, 2020 kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere (SabaSaba), Barabara la Kilwa Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka Leo, 07 Decemba 2020 (Picha na Eliud Rwechungura)

Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya bluu bahali) akipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam wakati alipotembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 -9 Desemba, 2020 kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere (SabaSaba), Barabara la Kilwa Dar es Salaam, kushoto ni mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka Leo, 07 Decemba 2020

Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya bluu bahali) akipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa kutoka kwa mjasiliamali mdogo wakati alipotembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 -9 Desemba, 2020 kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K.Nyerere (SabaSaba), Barabara la Kilwa Dar es Salaam, kulia ni mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka Leo, 07 Decemba 2020

Na Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara

Mhe Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb), Waziri Mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara ametembelea Maonesho ya tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yenye lengo la kujenga jukwaa kwa wadau wa sekta ya viwanda,  kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo katika sekta hiyo yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere (SabaSaba) tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020

Mhe Waziri mteule ameeleza kuwa lengo la kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ni kujifunza, kujionea bidhaa zinazolishwa na viwanda vyetu vya ndani, kujua bidhaa zinazotengenezwa, aina ya bidhaa hizo na kufahamu upatikanaji wa malighafi, kujua muunganiko wa uzalishaji pamoja na masoko.   

 “Nimepata faraja kuona mwamko mkubwa wa Watanzania kuweza kuzalisha bidhaa za Tanzania ambapo awali bidhaa hizo tulikuwa tunaagiza kutoka nje ya nchi, kupitia Maonesho nimeona dhamira yao na imenipa somo la kuona uhitaji wa uzalishaji mkubwa ili kuweza kusafirisha nje ya nchi” amesema Mhe Mwambe

Ameongeza kwa kusema kuwa nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hivyo wazalishaji wakiwezeshwa kwa kupata kipato kikubwa, wastani  wa mapato utaongezeka na kuwa juu hivyo juhudi ya pamoja ndani ya serikali kuelekea mwaka 2025 nchi itaingia kwenye uchumi wa kipato cha kati cha juu utakaopelekea kuboresha maisha ya Watanzania na kutengeneza uchumi wa viwanda ulioimara wenye muunganiko mzuri kati ya wazalishaji wa kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na masoko   

Amehitimisha kwa kusema kuwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara utatengenezwa mfumo thabiti wa kufanya muunganiko huo kupitia wizara zinazowagusa moja kwa moja ili kutengeza muunganiko wa wazi na matokeo makubwa na chanya.

MWISHO

No comments:

Post a Comment