Tuesday, December 8, 2020

MBUNGE WA KILOLO JUSTIN NYAMOGA AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI

 





MBUNGE wa Jimbo la Kilolo Mkoani Iringa Justin Nyamoga mekabidhi mifuko 70 ya Saruji yenye thamani ya Milioni 1.7 kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi shule ya Sekondari Ilindi iliyopo kata ya Mahenge iliyojengwa  kwa nguvu za wananchi.

Nyamoga amekabidhi msaada huo ikiwa ni Moja kutimiza ahadi yake  aliyoitoa wakati akiomba ridhaa ya  kuwa Mbunge wa Jimbo hilo katika  Kampeni ya uchaguzi Mkuu 2020.

Akizungumza na wananchi wa wakati wa kukabidhi msaada huo, Nyamoga amesema ataendelea kuipa kipaumbele sekta ya Elimu kwa kukamilisha Ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na kukarabati miundombinu ya shule zilizochakaa ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki.

No comments:

Post a Comment