Tuesday, November 17, 2020

WAANDISHI MOROGORO WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA UCHUNGUZI NA MISA TANZANIA

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya uandishi wa habari za kiuchunguzi na kuripoti Habari kwa mtazamo wakijinsia Bi. Dominica Haule ambaye pia ni Mwenyekitiwa GEMSAT akitoa elimu kwa washiriki kuhusu mbinu za ripoti habari kwa jicho la kijinsia.

Washirki wa mafunzo ya kuripoti habari za kiuchunguzi na mtazamo wa kijinsia yaliyoendeshwana MISA TAN mjini Morogoro hivi karibuni

Na Fredy Mgunda,Morogoro.

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya VIKES ya nchini Finland, imeandaa mafunzo ya kwa waandishi wa habari mkoa wa Mororgoro ili kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti habari za uchunguzi na kijinsia kwa weledi.

Mwenyekiti wa GEMSAT Bi. Dominica Haule alisema mafunzo hayo pia yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika mkoa wa Morogoro ili kuibua na kuripoti habari mbalimbali za kijinsia hususani zinazowagusa wanawake kwani wamekuwa hawapewi kipaumbele na vyombo vya habari.

“Tunahitaji kubadili fikra katika kuripoti habari za kijinsia, bado wanaume wanapewa kipaumbele huku wanawake wakisahaulika hivyo mafunzo haya yatusaidie kutoka tuliko na kuanza kuibua mambo mazuri yanayofanywa na wanawake na kuyaripoti kupitia vyombo vyetu vya habari”, amesisitiza

Alisema baadhi ya mila na desturi zimekuwa zikiathiri masuala mbalimbali ya usawa wa kijinsia hivyo waandishi wa habari wanapaswa kutumia vyombo vya habari kubadili hali hiyo ili kuleta usawa kwenye masuala ya kijinsia.

“Ili kurudisha imani hiyo ni lazima waandishi wa habari na vyombo vya habari kuiishi misingi au miiko ya wanahabari ambayo ni ukweli na usahihi, uhuru (kutokuwa tegemezi), kuzingatia usawa utu na uwajibikaji.

Haule alihimiza waandishi wa habari kuiishi misingi hiyo ikiwemo ukweli na usahihi bila kupendelea kwani wamepewa dhamana kubwa katika jamii.

“Kuna wasiwasi mkubwa kwa sasa juu ya utendaji wa wanahabari ambapo ukweli ni kwamba jamii haituamini tena. Lakini imani au kuaminika ni jambo la muhimu katika kazi yetu kama wanahabari” 

Kwa upande wake afisa habari na utafiti Neema kasabuliro alisema kuwa Mafunzo hayo yaliyoshirikisha waandishi wa Habari ishirini na mbili (22) yaliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa Habari nchini kuhusu mbinu za kuripoti Habari za kiuchunguzi pamoja na mtazamo wa kijinsia. 

Alisema kuwa mafunzo hayo yaliyofanyika siku 2 kuhusu uandishi Habari za kiuchunguzi na kuripoti Habari kwa mtazamo wa kijinsia yaliyoandaliwa na MISA TAN kwa ushirikiano na VIKES yaliyo fanyikia mkoani Morogoro kwa lengo la kuwaongezea uwezo waandishi hao. 

Wakati wa mafunzo hayo washiriki walijifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji, uandaaji na kuripoti Habari na taarifa zenye ushahidi wa kutosha na kwa kuzingatia muktadha wa kijinsia ili kuleta uwiano sahihi wa sauti za wanawake na wanaume kusikika. 

Washiriki wameishukru taasisi ya MISA Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo wakisema yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kuandaa habari na makala mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia kwa kutoa nafasi sawa baina ya wanawake na wanaume tofauti na ilivyo sasa ambapo asilimia kubwa ya vyanzo vyao ni wanaume wakati kuna wanawake wengi wanafanya mambo makubwa lakini habari zao hazipati nafasi.

No comments:

Post a Comment