Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akitoa maelezo ya namna gani ya kuzipata tofali kwa ajili ya kuhifadhi kwenye kila kijiji au mtaa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amewataka viongozi
wote wa vijiji na mitaa katika mkoa wa Iringa kuhakikisha wanakuwa na benki ya
Tofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na majengo ya serikali
pale yanapo hitajika.
Akiwa katika ziara ya Iringa mpya awamu ya pili
kutokana na uchakavu wa majengo mengi ya shule za msingi na vyumba vya madarasa,nyumba
za wafanyakazi wa kada mbalimbali wa serikali katika maeneo husika kuna haja ya
kuweka mkakati wa kuanzisha benk ya tofali ili kuboresha na kuanzisha majengo
mapya katika maeneo husika.
“Naagiza viongozi wote kuhakikisha wanasimamia wananchi
kufyatua tofali za kutosha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo mbalimbali
katika vijiji au mitaa husika pale panapo hitajika” alisema Hapi
Alisema kuwa umuhimu wa benki ya tofali na pale inapotokea
kuna upungufu wa majengo kwa ajili ya matumizi ya kiserikali inakuwa kazi
rahisi kuanzisha ujenzi wa majengo au jingo husika kwa kuwa tayari tofali zipo.
Aidha Hapi aliwaagiza wakurugenzi wote wa mkoa wa
Iringa kuhakikisha wanaandika andiko kwa ajili ya kuombe fedha kwaajili ya
shule zote zilizojengwa miaka ya 1960 kwa kuwa miundombinu yao kwa sasa haipo
vizuri.
Katika ziara yangu nimekugundua kuwa fedha za lipa
kulingana na matokeo (EP4R) zimetumika vizuri na kuleta matokeo chanya katika
mkoa wetu wa Iringa,kwani majengo mengi yamejengwa kwa viwango vianavyotakiwa.
No comments:
Post a Comment