March 2, 2020 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ametimiza ahadi yake kwa kuwakabidhi Mama lishe wa Stendi kuu ya mabasi Mbeya jiji vitendea kazi maalum vya kutumia wakati wa kuhudumia wateja wao (Aprons) ambapo jumla ya vitendea kazi vimetolewa, pamoja na hilo Dkt. Tulia ametimiza pia ahadi ya kutoa TV ambayo itakuwa inawawezesha abiria wa kituo hicho kufuatilia matukio mbalimbali pamoja na habari wakati wakisubiri kusafiri.
“Siku ya leo hatujaja kutekeleza kila ahadi kwasababu hapa tuna machinga ambao nao pia wanasubiri baadhi ya ahadi tulizozitoa lakini wakati tukiendela kuvuta subira hizo tumekuja kuwakabidhi mama lishe Aprons 200 kwa ajili ya kulinda nguo zao pamoja na kukaa katika hali ya usafi”
“Lakini pia tulipokuja kukabidhi jezi kwa ajili ya maafisa usafirishaji tulisomewa changamoto nyingine ikiwemo watu kupata taarifa mbalimbali kwahiyo siku ya leo tumeweza kuleta pia TV ukizingatia kwasasa tunaye kijana wetu Mbwana Samatta akikipiga kule Aston Villa naye tutakuwa tunaweza kumtazama lakini pia na taarifa nyingine za habari zikiwemo zinazomuhusu Rais wetu mpendwa Magufuli na Serikali yake”-Dkt. Tulia Ackson Cc @tulia.ackson
No comments:
Post a Comment