Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 3 Februari 2020 wakati wa mkutano wa kumi na nane.
Na Mathias Canal,
Wizara ya kilimo-Dodoma
Kutokana
na kuwepo kwa upungufu wa pembejeo nchini, Serikali imechukua hatua mbalimbali
za kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wingi ili kutosheleza mahitaji ya
ndani ya nchi.
Hatua
hizo ni pamoja na; kutoa vibali kwa wasambazaji wakubwa wa mbolea kuagiza nje
ya mfumo wa BPS kutokana na mahitaji ya wakulima na soko ambapo tani 200,000
zimeagizwa na hadi kufikia tarehe 30 Januari, 2020; Kutoa kibali cha kuagiza
tani 45,000 kwa Umoja wa wasambazaji na wauzaji wa pembejeo za kilimo; na
kuagiza mbolea tani 43,000 kwa kutumia mfumo wa BPS ambapo mbolea hiyo imeanza
kusambaza nchini tangu tarehe 28 Januari, 2020.
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo tarehe 3 Februari 2020 bungeni Jijini
Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe Dkt. Pudeciana
Wilfred Kikwembe aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani juu ya
ucheleweshwaji wa pembejeo za kilimo hasa mbegu na mbolea ambazo huwasababishia
wakulima hasara.
Mhe
Mgumba amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuboresha
mifumo ya uzalishaji, udhibiti na usambazaji wa pembejeo nchini ambapo sekta ya
Umma na binafsi zitashirikishwa na kuhamasishwa kuzalisha pembejeo nchini ili
kukidhi mahitaji.
Kuhusu
upungufu wa mbolea nchini Mhe Mgumba amesema kuwa umechangiwa na sababu
mbalimbali ikiwemo kuchelewa kupatikana kwa mahitaji kutoka kwa Makampuni ya
mbolea hapa nchini, kuongezeka kwa matumizi ya mbolea kutokana na bei nzuri ya
mazao kwa msimu wa 2018/2019; kuongezeka kwa kilimo cha kibiashara baada ya
Serikali kuwahakikishia wakulima kuwa haitafunga mipaka na kuingilia upangaji
wa bei za mazao ya kilimo na kuwepo kwa mvua nyingi ambazo zimesababisha
kuongezeka kwa viwango vya matumizi ya mbolea kwa wakulima.
Katika
msimu wa 2019/2020 upatikanaji wa pembejeo zikiwemo mbegu bora hadi kufikia
Desemba, 2019 ni tani 71,155.13.
Kati ya hizo, tani 58,509.9
zimezalishwa nchini, tani 5,175.79 zimeingizwa kutoka nje ya nchi na tani 7,469.44 ni bakaa ya msimu 2018/2019.
Aidha,
upatikanaji wa mbolea hadi kufikia tarehe 30 Januari, 2020 ni tani 410,499
zikijumuisha tani 92,328 za UREA na tani 84,311 za DAP. Kati ya hizo tani
225,417 zimeingizwa kutoka nje ya nchi, tani 16,685 zimezalishwa ndani ya nchi
na tani 168,397 ni bakaa ya msimu wa 2018/2019.
MWISHO
No comments:
Post a Comment