Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mzee Zefania Kanoge Petro 82 ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Mzee Kanoge ndiye aliyemshawishi Mhe.Rais Dkt. Magufuli kuingia kwenye Siasa wakati alipokuwa akifanyakazi katika Mkoa wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano ya Chato wakati wakati alipowakuta katika Kiliniki wa Baba Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Chato wakisubiri kuchomwa Sindano za Chanjo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wazazi waliowapeleka watoto wao kupewa chanjo katika Kliniki ya Baba Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali pamoja na Madaktari wa Hospitali hiyo ya Chato mara baada ya kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kutembelea Kliniki ya Watoto hospitalini hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafiwa katika msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge aliyefariki tarehe 4/11/2019 na anatarajiwa kuzikwa kesho Choto mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwanunulia madaftari wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Ladislaus , Daudi Petro na Shemila Mlegete mara baada ya kukutana nao katika eneo la Chato mjini wakati wakitokea shuleni kwao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Shangazi yake Salome Michael Nyahinga katika eneo la Chato wakati akitokea kuhani Msiba wa Mzee Mariganya Nghwenge katika eneo la Ginnery Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkazi wa Chato Venance Magege wakati aliposimama kuwasalimia wananchi wa Chato mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Chato mjini mara baada ya kusimama kuwasalimia wakati akitokea kuhani msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge katika eneo la Ginnery Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Shemla Mlegete wakwanza kushoto, Ladislaus katikati pamoja na Daudi Petro mara baada ya kuwaona wakati akitoka akizungumza na wananchi wa Chato.
Picha ya Kumbukumbu- Marehemu mzee Mariganya Nghwenge aliyefariki juzi akiwa ameshikilia Mhogo mrefu alipokuwa akimuonesha Rais wa kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere (haonekani pichani) mwaka 1967 katika eneo la Ginnery Chato mkoani Geita. Mzee huyo alikuwa akionesha namna gani alikuwa Mkulima bora katika kipindi hicho.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment