Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akitoa
ufafanuzi wa hoja zilizojitokeza katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na
Wawekezaji katika ukumbi wa Chuo cha Wauguzi Kibaha Pwani.
Mmoja
ya washiriki wa Mkutano akiwasilisha hoja yake mbele ya jopo la Mawaziri na
Manaibu Waziri walioshiriki Mkutano wa
Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji katika ukumbi wa Chuo
cha Wauguzi Kibaha Pwani.
Na Lulu Mussa, Pwani
Serikali
imesema kamwe haitaruhusu uzalishaji, uingizaji na matumizi ya mifuko mbadala
aina ya Non-Woven isiyokidhi viwango
vya 70 Gram Per Square Metre (GSM)
kutumika nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mussa Sima katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali,
Wafanyabiashara na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua
changamoto zao, Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha
mkoa wa Pwani.
Awali
akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo
amesema kuwa kumekuwa na uchelewashaji wa utoaji wa vibali vya kuingiza mifuko
mbadala nchini kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira hali
ambayo inaleta vikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Akitoa
ufafanuzi wa ucheleweshaji wa vibali hivyo Mhe. Sima amesema kuwa Serikali
imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini tangu Juni Mosi 2019 na
kutoa fursa kwa wakezaji kuagiza na kuzalisha mifuko mbadala ili kukidhi soko
la ndani.
Hata hivyo changamoto imejitokeza kwa
wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuingiza mifuko isiyokidhi viwango aina
ya Non-Woven. “Kumeanza kujitokeza
uvunjifu wa sheria katika uzalishaji na uingizaji wa mifuko mbadala aina ya non-woven. Shirika la Viwango Tanzania
(TBS) limeweka vigezo vya mifuko mbadala aina ya non-woven inayoweza kutumika nchini ikiwa ni pamoja na Uzito
usiopungua GSM 70 (Gram per Square Metre), iweze kurejelezwa, Ioneshe uwezo wa
kubeba, anuani ya mzalishaji na iwe imethibishwa na Shirika la Viwango Tanzania
(TBS)” Sima alifafanua.
Amesisitiza busara itumike katika kumaliza
mgogoro uliopo baina ya mfanyabiashara aliyeagiza bidhaa hiyo huo bila kuathiri
upande wowote kwa kutoa mapendekezo kwa mfanyabiashara mwenye mzigo husika
kuurejereza ama kuusafirisha nje ya chini ya uangalizi maalumu na kuagiza
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Shirika la
Viwango nchini (TBS) kumaliza suala hilo mapema iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Sima
amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya mapitio ya Kanuni za Taka
Hatarishi za mwaka 2009 na kutunga Kanuni mpya ya mwaka 2019 ambazo
zimezingatia Mkataba wa Basel yaani Basel
Convention for transboundary Movement of Hazadous Waste ambao Tanzania
imeridhia baada ya awali biashara hiyo hairatibiwi ipasavyo
“Kwa mujibu wa Mkataba huu, mfanyabiashara
anapotaka kuingiza Hazadous Waster ikiwemo chuma chakavu pamoja na masharti
mengine ni lazima nchi ambapo chuma chakavu kinatoka kupata kibali cha Serikali
ya nchi husika ili kuthibitisha kuwa nchi hiyo imeruhusu usafirishaji huo” Sima
alisisitiza.
Amefafanua kuwa malighafi inayotumika na
Viwanda vya ndani imekuwa ikipelekwa nje, hivyo Serikali imeweka masharti magumu kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani
na kuruhusu kusafirishwa kwa malighafi ambayo haitumiki hapa nchini.
Naibu Waziri Sima amewahimiza wawekezaji
kuwekeza katika Mkoa wa Pwani na kutumia nishati ya gesi kwa wingi. “Ni viwanda
48 tu nchi nzima ndio vinatumia nishati ya gesi, wawekezaji wekeni nia ya
matumizi ya Gesi ili TPDC waweke miundombinu stahiki, nawasihi ndugu zangu
tulinde mazingira yetu”
Siku ya
pili ya mkutano wa Mkutano wa Mashauriano
baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji umefanyika katika ukumbi wa
Chuo cha Uuguzi Kibaha mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na washiriki kutoka
Wilaya zote za Mkoa wa Pwani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment