Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga
akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, kulia ni Naibu Waziri wa
Kilimo, Hussein Bashe, na kushoto ni Naibu Waziri mwingine wa Wizara hiyo,
Omary Mgumba
Wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa
Kilimo, Mhe Japhet Hasunga leo jijini Dodoma
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wandishi
wa habari leo jijini Dodoma, pengine yake ni manaibu Waziri wa Wizara hiyo,
Hussein Bashe na Omary Mgumba
Waziri wa
Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake
jijini Dodoma leo.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga
amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya
uchunguzi kwenye mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho baada ya kubaini
kuwepo na udanganyifu.
Mhe Hasunga amemuagiza CAG
kuchunguza kiasi cha Shilingi Bilioni 53.2 kilichobaki kwenye akaunti ya Mfuko
wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho ambazo zilikuwa kwa ajili ya kujenga
viwanda vitatu vya kubangua korosho na maghala.
Aidha Mhe Waziri ameunda timu ya watu wasiozidi watano kwa ajili ya kuhakiki kiasi cha korosho kilichopokelewa na kilichouzwa katika msimu wa Korosho wa mwaka 2018/2019 baada ya kubaini uwepo wa udanganyifu.
Hayo ameyasema leo tarehe 17 Novemba 2019 jijini Dodoma mbele ya wandishi wa habari ambapo amezitaka pia kamati za ulinzi na usalama kusimamia zoezi la uhakiki ambalo linaonekana kutawaliwa na udanganyifu ambapo timu iliyoundwa itashirikiana na timu iliyokuwepo chini ya wizara hiyo kuhakiki pia fedha zilizopatikana ili wahakikishe wanaolipwa ni wale wanaostahili.
Aidha amesema timu hiyo ihakikishe kuwa majina yaliyotoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu hadi fedha zilizoingia benki kama kweli ziliingia kwenye akaunti za wakulima na kama kuna unyaufu uliojitokeza wabainishe ni kwa kiwango gani ili kusaidia serikali kutoa taarifa yenye uhalisia.
Waziri Hasunga amesema mwaka 2016 serikali iliamua kufuta mfuko wa Wakfu na kwenye akaunti kulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 53.2 lakini bodi ya Korosho iliamua kubadili matumizi na kutumia fedha hizo tofauti na maagizo yaliyotolewa na serikali.
"Kama Wizara hatupo tayari kuona ubadhilifu wowote wa fedha za umma unafanyika, Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali kuona watu wachache wanafaidika na fedha za walipa kodi wa Tanzania.
Timu zote mbili naziagiza hadi kufikia Januari 15 mwaka 2020 wawe wameshatuletea ripoti wizarani. Niwahakikishie hatutomvumilie yeyote ambaye atajaribu kugusa fedha za wananchi, " Amesema Waziri Hasunga.
Amesema bodi hiyo ilitumia kiasi cha shilingi bilioni 28.1 kununua viuatilifu,walitumia kiasi cha shilingi bilioni 12.2 kulipia magunia ilhali katika msimu huo wanunuzi walikuwa wananunua magunia wao wenyewe.
Ametoa wito kwa wakulima kuwa kama kuna anayedai ushirika apelike madai yao kwenye kamati ya ulinzi na usalama na timu iliyoundwa ili waseme kama hawajalipwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment