Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda akizungumza mbele ya Viongozi wa dini katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam leo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini hapa nchini katika
Mkutano uliowahusisha viongozi hao pamoja na Mkuu wa Mkoa huyu katika
ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
leo.
Viongozi wa Dini Mbalimbali hapa
nchini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Paul Makonda
katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es
Salaam leo.
**********************************
Viongozi wa Dini wakiwemo
Maaskofu, Mashekhe, Wachungaji,Manabii, Maimamu na Wainjilisti Mkoa wa
Dar es salaam leo November 18 wametoka na azimio la pamoja la kumuunga
Mkono Rais Dkt. John Magufuli katika jitiada zake za kuleta maendeleo
kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kumaliza kero za
Wananchi.
Hatua ya Viongozi hao wa dini
imekuja baada ya Kuvutiwa na taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam Mhe. Paul Makonda dhidi ya Miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa kwenye Mkoa huo chini uongozi thabiti wa Rais Dkt. John
Magufuli jambo lililowakosha Viongozi wa Dini na Kuamua kuja na tamko
hilo.
Katika mkutano huo RC Makonda
amewasilisha kwa Uhalisia wa Video taarifa ya miradi iliyotekelezwa na
serikali katika sekta zote muhimu ikiwemo Afya, Barabara, Maji, Umeme,
Elimu, Viwanda, Usafirishaji na sekta anyinginezo jambo lilikowagusa
viongozi wa dini.
Pamoja na hayo Viongozi hao wa
Dini wamesema wataendelea kumuombea Rais Dkt. John Magufuli azidi kuwa
na Nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi.
No comments:
Post a Comment