Waziri wa Afya Maeandeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango
wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Semima
iliyofanyika jijini Dodoma.
Mshauri Mbobezi wa Sera na Mipango
kutoka Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Usu Mallya
akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii kuhusu Mpango wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na
katika Semima iliyofanyika jijini Dodoma.
Baaadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo
kuhusu Mpango wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na katika
Semima iliyofanyika jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Maeandeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Mwaka
2017 Tanzania ilikuwa na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
takribani 41elfu na kati ya vitendo hivyo ukatili dhidi ya watoto
pekee ni 13 elfu.
Naibu Waziri Ndugulile amesema
hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Semina ya
wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mkakati wa
Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
Jijini Dodoma.
Aidha Naibu Waziri Ndugulile
ameifananisha changamoto ya vitendo vya ukatili Nchini kuwa ni ujambazi
mpya unaozidi kuwakumba wanawake na watoto kutokana na vitendo hivyo
kuendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Dkt. Ndugulile amesema
unapoongelea ukatili wa kijinsia unazungumzia maeneo makubwa matatu
ambayo ni ukatili wa kimwili, kisaikolojia na ukatili wa kiakili na
kuongeza kuwa changamoto ya ukatili wa kijinsia imekuwa ikiongezeka
mwaka hadi mwaka.
Ameyataja matendo hayo yanayozidi
kuongezeka kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, ubakaji na ulawiti dhidi ya
wanawake na watoto ndio maana ili kukabiliana na vitendo hivyo serikali
tangu mwaka 2016 ilianzisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa
juhudi za Serikali katika utoaji elimu bure hapa nchini umepunguza suala
la mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa mtoto wa kike anapozidi kukaa
shuleni ndivyo uwezekano wa mimba za mapema unapozidi kuwa mdogo.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter
Serukamba amewambia wajumbe wa Kamati hiyo na Wizara kuwa jamii bado ina
mila potofu zinazoendeleza vitendo vya ukatili kama vile ukeketeji na
kuwataka Wabunge kuelimisha Jamii dhidi ya Vitendo hivyo.
Aidha Mhe. Serukamba amelitaja
suala la elimu kwa umma kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukatili kupewa
kipaumbelae huku akisifu mpango wa Serikali wa kutokomeza umasikini kwa
kiwango cha kaya kupitia TASAF na kuongeza kuwa umasikini pia ni chanzo
cha ukatili dhidi ya wawanawake na watoto.
Naye Mshauri Mbobezi wa Sera na
Mipango kutoka Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Usu
Malya amesema shirika lake litaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya
Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya
Wanawake na Watoto hapa nchini.
Mpango wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ulianza tangu mwaka 2016 na
umewezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika utekelezaji wa kutokomeza
ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuondoa mwingiliano, upotevu wa
rasilimali watu, fedha na muda unaotumika katika kushgulikia suala moja.
No comments:
Post a Comment