Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiangalia Mti wa Mkeshia
alioupanda kwenye eneo la Mzakwe Makotopora Jijini Dodoma wakati
alipofanya Ziara ya Kustukiza kuangalia maendeleo ya Ukuaji wa Miti 276
iliyopandwa katika eneo hilo leo Octoba 10,2019 ambapo ameridhika na
utunzaji wa Miti hiyo unaofanywa na Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa
JKT. Kulia Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi Kushoto
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhandisi Geoseph Malongo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza na Vijana wa
Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT Makutopora wanaohusika na Utunzaji
wa Miti iliyopandwa katika eneo la Mzakwe Makutopora Jijini Dodboma,
wakati alipofanya Ziara ya Kushtukiza kuangalia maendeleo ya Ukuaji wa
Miti 276 iliyopandwa katika eneo hilo leo Octoba 10,2019 ambapo
ameridhika na utunzaji wa Miti hiyo.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimsikiliza
Imakulata Yoram (36) Mkazi wa Nkuhungu Dodoma aliyejifunguwa mtoto wa
kike katika Hospitali ya Mkoa Dodoma wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza kuangalia Changamoto mbali mbali ziliopo kwenye Hospitali
hiyo leo Octoba 10,20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimsikiliza Mtoto Ernest
Michael (6) Mkazi wa Nkuhungu Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa
Dodoma kwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuangalia
Changamoto mbali mbali ziliopo kwenye Hospitali hiyo leo Octoba 10,2019.
kulia Michael Yohana Baba wa Mtoto huyo.
*******************************************
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amemuagiza
Meneja Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Misitu TFS Kanda ya kati
Dodoma Bibi Tebby Yoramu kufuatilia Utafiti wa Udongo kwenye eneo la
Mzakwe Makutopora Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais
ameyasema hayo leo wakati alipofanya Ziara ya kushtukiza kuona maendeleo
ya ukuaji wa Miti ya aina mbalimbali iliyopandwa katika eneo lindwa la
Hifadhi ya Chanzo cha Maji linalotunzwa na Jeshi la kujenda Taifa JKT
Makutopora ambapo amesema kuwa azma ya kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani
ipo pale pale.
Makamu wa Rais
ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora, Wakala wa Misitu
Tanzania na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti iliyopandwa
mwezi Desemba 2017 inastawi Vizuri.
“Vitabu vya dini
vinasema Moja kati ya sadaka endelevu ni kupanda miti, miti hii imekuwa
na kustawi kwasababu ya jitihada zenu za kuimwagilia na kuitunza,
msikate tamaa, endeleeni na kazi hii njema ambayo matokeo yake
yanaonekana ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mifumo ya hali ya hewa
ambayo huimarisha shughuli za kilimo na maendeleo ya viwanda.”
Alisisitiza Makamu wa Rais
Nae Mkuu wa Kambi
ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali Festo Mbanga amesema kuwa miti
2300 ilipandwa tarehe 21/12/2017 na kati ya hiyo miti 2076 imekuwa na
kustawi ikiwa ni sawa na asilimia 90.3 ya miti yote iliyopandwa.
“Katika miti
iliyooteshwa awali baadhi haikuota, hivyo tumefanya jitihada za
kuirudishia, tumepanda takriban miti 300 ya ziada” alisema Luteni Kanali
Mbanga.
Katika hatua
nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)
kuhakikisha tafiti zinakamilika mapema kutoka katika sampuli ya udongo
iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika eneo hilo na
Jiji la Dodoma kwa Ujumla.
Kampeni ya
Kukijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania tarehe 21/12/2017 katika eneo la Mzakwe Jijini Dodoma
ambapo miti 2300 ilipandwa siku hiyo.
Hayo yamesemwa
leo mara baada ya kutembelea shamba la miti lililopo katika eneo la
Mzakwe katika Kambi ya Jeshi la Makutupora Jijini Dodoma, ikiwa ni
ufuatiliaji wa Kampeni aliyozindua mwaka 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya
kijani.
Wakati huo huo
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya Ziara ya Kushtukiza
katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuangalia Changamoto mbalimbali
ziliopo kwenye Hospitali hiyo, na kuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo
kushuhulikia na kusimamia vizuri matumizi ya fedha kwa ajili ya mahitaji
yaliyopangwa.
No comments:
Post a Comment