Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kwa
kupitia taasisi yake ya Tulia Trust amefanya ziara katika shule
mbalimbali mkoani Mbeya lengo likiwa ni kusaidia kuboresha miundombinu
ya elimu ambapo miongoni mwa shule hizo ni pamoja na Shule ya msingi
Jitegemee ambayo ameipa mchango wa Shilingi Milioni mbili (Tsh
2,000,000/-) ili kusaidia ukarabati wa miundombinu mibovu katika shule
hiyo.
Pia, baada ya kusomewa changamoto
nyingine zikiwemo ubovu wa madarasa, ukosefu wa uzio na ofisi za
waalimu, Dr. Tulia ameahidi kutoa msaada zaidi kwenye shule hiyo kwa
kupitia taasisi yake ya Tulia Trust.
Katika hatua nyingine, Dr. Tulia
ametoa mchango wa Shilingi Milion moja na laki sita (Tsh 1,600,000/-)
katika Shule ya Msingi Nzovwe iliyopo Jijini Mbeya ili kusaidia pia
uboreshaji wa miundombinu isiyo rafiki katika shule hiyo ambapo pia
alisomewa changamto zingine ikiwemo ubovu wa madarasa, uzio wa shule n.k
“Nimesomewa changamoto nyingi
zilizopo katika shule zetu hizi ambapo niseme tu sisi kama Tulia Trust
tumezipokea na tutaenda kuona ni namna gani basi tunaweza kuzifanyia
kazi ili basi watoto wetu hawa waweze kuzoma katika mazingira yaliyo
bora na salama”-Dr. Tulia
No comments:
Post a Comment