Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Tuzo ya Shukurani, Mkurugenzi Mkuu wa Makmpuni ya ASAS,
Salim Abri kutokana na mchango wake mkubwa katika huduma mbalimbali za
jamii mkoani Iringa. Tuzo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Mji wa
Iringa. Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa CCM Mkoa wa
Iringa, Mizengo Pinda, wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofis ya Waziri
Mkuu, Stella Ikupa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili
kwenye uwanja wa Kichangni Kihesa mjini Iringa kuzindua Kambi ya Kutoa
Huduma za Afya kwa Wazee na Walemavu, Septemba 29, 2019. Wa pili
kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi
akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozindua Kambi ya
Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa
Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapngia wazee wakati alipozindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa
Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa,
Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua
Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja
wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na wazee waliojitokeza
kupata huduma za tiba na vipimo wakati Waziri Mkuu alipozindua
Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja
wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu) .
No comments:
Post a Comment