Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo katika Mkutano wake na
Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini,
mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanachama wa Chama wa
Washereheshaji (SAA) wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko
mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Msanii wa Bongo Movie Nchini, Muhogo
Mchungu akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia
hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Bongo Movie Nchini, Simoni
Mwapagata akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia
hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Bongo Movie, Shemsa Ford
(kulia) na Jackline Wolper (kushoto) wakiteta jambo kabla ya Mkutano wa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe,
na Wasanii wa Sanaa zote nchini kuanza katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, akiandika mapendekezo anayoyasikia
kuhusu mabadiliko ya Taasisi za Sanaa nchini katika Mkutano wake na
Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini,
mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
…………..
Na Dianarose Shirima-MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amekutana na wadau wa Sanaa mbalimbali
nchini katika kujadili maendeleo ya tasnia hiyo, zikiwepo haki za
wasanii na jinsi ya kuboresha tasnia ya Sanaa na muziki ili wasanii
waweze kufaidika kwa kile wanachokifanya
Akizungumza katika Mkutano huo Waziri
Mwakyembe amesema kuwa Serikali ipo tayari kupokea mapendekezo ya
wasanii kuhusu kuunganisha nguvu katika vyombo vya wasanii ambavyo ni
COSOTA, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) NA Bodi ya Filamu Tanzania ili
waweze kuhudumia wasanii kwa maendeleo ya kazi zao.
“Sisi tunawaletea mawazo tu, si Sheria, si
Mswada ni mawazo ambayo yatamilikiwa na ninyi baada ya kuyapitisha”, na
ninyi kama wadau wa Sanaa na muziki waliohudhuria kwenye mkutano huu
mntakia kutoa mawazo yenu ili Tasnia hii iweze kufikia katika muafaka
mzuri ambao utaboresha kazi za wasanii na kutetea maslahi ya kazi zao,
Alisema Dkt.Mwakyembe.
Dkt. Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya
Sanaa na Mziki imekuwepo muda mrefu na imekuwa kimbilio kwa vijana
wengi, lakini imekuwa ikitajirisha baadhi ya watu na wengine kuachwa
nyuma kimaendeleo, kwa hiyo mabadiliko katika Tasnia hiyo hayana budi
kutokea ili kuleta ufanisi zaidi
Aliongeza kuwa mabadiliko hayo hayalengi
kuvunja au kuingilia Mamlaka ya vyombo hivyo, bali lengo lake ni
kusogeza huduma karibu kwa ajili ya kurahisisha kazi kwa wasanii na
wadau wote wa Sanaa nchini.
Aidha Dkt.Mwakyembe alisema kuwa
mabadiliko hayo yatafanya vyombo hivyo kuwa na lugha moja ili kuepuka
wasanii kukamatwa au kufungiwa pale wanapokuwa wanafanya kazi zao
kutokana na utofauti wa kanuni na Sheria zilizopo.
“Kipindi cha mabadiliko kimefika,
watanzania tusiogope kufikiri katika tasnia hii, kwa muda mrefu imekuwa
ikisaidia sana lakini haiwezi kuwafaidisha wachache na wengine wabaki
masikini, haiwezekani ni lazima tufikirie njia itakayo tusaidia wote”,
alisema Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la
Sanaa za Maonyesho Tanzania, William Frank Chitanda, alisema kuwa
Mabadiliko ya kuiunganisha Basata na Bodi ya Filamu ziungane na COSOTA
ihamishiwe Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Wizara ya
Viwanda na Biashara.
No comments:
Post a Comment