Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na vijana wa Mkoa wa Geita alipokuwa
akizindua Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara
kwa vijana inayoratibiwa na kusimamiwa na ofisi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale
Mhe. Hamim Gwiyama akitoa taarifa fupi kuhusu fursa zilizopo katika Mkoa
wa Geita zinazoweza kuwanufaisha vijana wa mkoa huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akielezea kuhusu
Programu hiyo ya ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa
Geita ambapo vijana 150 walihudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sehemu ya Vijana Wajasiriamali
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo
Mkoani Geita.
Baadhi ya vijana wajasiriamali
wakimsikilza kwa makini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani) alipokuwa akizindua awamu ya tatu ya utekelezaji wa
Programu ya Mafunzo na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa
Geita.
Sehemu ya Kamati ya Ulinzi na
Usalama wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo
yaliyofanyika Mkoani Geita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akigawa cheti cha Ushiriki kwa mmoja wa vijana
aliyeshiriki katika mafunzo hayo Bw. Daniel Ntigizu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana alipokuwa
akizindua awamu ya tatu ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo na
Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa Geita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawezeshaji wa
Mafunzo ya Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe.
Hamim Gwiyama mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo kwa ajili ya
uzinduzi wa awamu ya tatu ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo na
Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa Geita. Kulia ni Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa huo Bw. Deogratius Kayango.
…………………………………………………..
Na; Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu imedhamiria kuwawezesha vijana kupitia programu ya mafunzo ya
Ujasiriamali na Usimamaizi wa Biashara kwa lengo la kuwawezesha kukuza
na kurasimisha biashara zao.
Akizungumza wakati wa hafla fupi
ya uzinduzi wa programu ya mafunzo hayo katika Mkoa wa Geita Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa mafunzo hayo ni
mahususi kwa vijana na yatawawezesha vijana kupata elimu juu ya masuala
mbalimbali ya ujasiriamali na biashara ikiwemo urasimishaji wa
biashara, kutambua ushindani, upatikanaji wa mitaji, masuala ya
uchambuzi wa masoko, mikakati na uendeshaji wa biashara.
“Mafunzo haya yanamanufaa sana
kwenu ninyi vijana kwa kuwa yatawawezesha kukua kwa kasi katika biashara
zenu mnazoziendesha na hivyo kuwajengea wigo mpana wa kuendeleza
shughuli za kiuchumi mnazozifanya,” alisema Mhagama
Alifafanua kuwa Ujasirimali ni
moja ya nguzo za sera ya taifa ya uwezeshaji ambayo inalenga kuinua
viwango vya ujuzi na uzoefu wa masuala ya biashara nchini.
Alieleza kuwa, kupitia programu
hiyo vijana 4,000 watanufaika na Mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo
vijana nchini kuwa na uelewa juu ya masuala ya biashara ikionesha
utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe.
Rais, Dkt. John Magufuli katika kuwawezesha vijana.
“Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea
kuwajengea uwezo vijana kote nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
katika kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kujiajiri, kuajiri
wenzao kwa ujumla pamoja,” alisisitiza Mhagama
Aliongeza kuwa dhamira ya
Serikali katika kuwawezesha vijana inatekelezwa kwa vitendo kupitia
programu mbalimbali ikiwemo ya ukuzaji ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, mmoja wapo ikiwemo ya Mafunzo ya Ujasirimali kwa vijana.
Sambamba na hayo, Mhe. Mhagama
aliwasihi vijana walioshiriki mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kuwa ni
chachu ya mageuzi katika kuboresha biashara zao. Pia aliwataka vijana
hao kueneza ujuzi waliopata kupitia mafunzo hayo kwa vijana wenzao.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa
maagizo kwa viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha vijana wanashiriki kwa
wingi katoka mafunzo hayo kwa kuwa yataleta matokeo chanya kwa jamii na
yatakuwa ni chachu kwa vijana katika kujiletea maendeleo sambamba na
kuwawezesha kuchangia pato la Taifa.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya
Nyang’hwale Mhe. Hamim Gwiyama ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo
alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana maana wao ndio nguvu
kazi ya taifa, hivyo kijana akiwa na ujuzi wa mambo mbalimbali ya
biashara ni faida kwake kutambua njia bora za kukuza shughuli zao za
uzalishaji mali.
“Katika Mkoa wa Geita vijana
walikuwa na mawazo kuwa dhahabu ndio biashara pekee itakayowapa faida,
ila kupitia mafunzo haya wataweza kutambua kuwa biashara yoyote
wakisimamia vizuri itakuwa na manufaa kwao,” alisema Gwiyama
Naye, Mmoja wa Vijana
walioshiriki katika Mafunzo hayo Bw. Salim Hassan aliweza kutoa shukrani
zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yameweza kuwatoa
katika sehemu moja na kuwapeleka hatua nyingine.
“Leo tumepata stadi za msingi
katika masuala ya ujasirimali na biashara, tumeweza kuelewa umuhimu wa
kutunza kumbukumbu, usimamizi wa fedha, taratibu za kurasimisha biashara
na jinsi ya kutafuta masoko,” alisema Hassan
Programu ya Mafunzo ya
Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara ilizinduliwa rasmi na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Jijini Dodoma Julai 29,
2019. Mafunzo hayo yanasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana
na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika Mikoa
nane (8) ya Tanzania Bara ikiwemo Dodoma, Ruvuma, Geita, Mwanza, Lindi,
Mbeya, Arusha na Tanga. Tayari vijana kutoka Mkoa wa Dodoma na Ruvuma
wamekishwa nufaika na mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment