Wednesday, August 21, 2019

MHE HASUNGA AFANYA MIKUTANO SABA JIMBONI, AELEZA MAMBO MSINGI YALIYOFANYWA NA DKT MAGUFULI KWA KIPINDI KIFUPI

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo jana tarehe 22 Agosti 2019 wakati akizungumza wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Mtaa wa Mantengu A kata ya Vwawa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakazi wa mtaa wa Mantengu B kata ya Vwawa wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo jana tarehe 22 Agosti 2019 wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo jana tarehe 22 Agosti 2019 wakati akizungumza wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Mtaa wa Mantengu A kata ya Vwawa.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua mradi wa maji Vwawa jana tarehe 22 Agosti 2019 wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo ikiwemo matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Vwawa amewaeleza wananchi mambo manne ya muhimu ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi cha muda mfupi tangu aingie madarakani Octoba 2015.

Mambo hayo muhimu aliyowaeleza wapiga kura wake ni pamoja na Ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika Mto Rufiji.

Alisema kuwa Mradi huo unajengwa kwa fedha za ndani upo katika eneo la Selous ambalo ni moja ya maeneo ya turathi za dunia, Mradi huo ambao unafahamika pia kwa jina la Stieglers Gorge, unatazamiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme, hatua ambayo ameeleza kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii. Hivyo Tanzania kuwa na utoshelevu wa umeme.

Mhe Hasunga ameeleza pia kuhusu Ujenzi wa reli ya kisasa, ambapo alisema kuwa nchi nyingi zilizoendelea duniani zinatumia reli kuchochea ukuaji uchumi na biashara kwa sababu usafirishaji kwa kutumia njia hiyo una uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kwa mara moja na kwa gharama nafuu kulinganisha na aina nyingine za usafirishaji.

Alisema, Serikali imedhamiria kujenga Reli ya Kisasa (SGR) kwa kiwango cha kimataifa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ndilo limepewa dhamana ya kusimamia mradi huo. Reli inayojengwa (Standard Gauge), yenye upana wa mita 1,435 ndio mfumo unaotumika sasa ukikadiriwa kuchukua asilimia 50 ya mitandao ya reli duniani.

Katika mikutano yake zaidi ya 24 aliyoifanya katika Jimbo hilo kwa takribani siku nne Mhe Hasunga ametaja pia juhudi za Rais Magufuli kwa kuamua kununua Ndege zaidi ya nane.

Alisema kuwa Miaka ya nyuma Kabla ya Rais wa Tanzania aliyopo sasa madarakani Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais, Shirika la ndege nchini Air Tanzania lililoanzishwa tangu Mwaka 1977 lilikuwa na Ndege moja aina ya Bombardier DASH8 Q300 ambayo ilikuwa ikihudumu tangu 2011. Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 na kuanza mkakati wa kulifufua Shirika hilo na kuonesha nia ya kununua ndege mpya za Tanzania.

Kuna Bombardier DASH8 Q400 tatu, mbili ambazo zilifika Tanzania Septemba 2016 na moja Juni 2017; Bombardier CS300 mbili na Boeing 787 Dreamliner ambazo zilitua Tanzania kati ya mei na Julai 2018. Ndege nyengine ni Airbus A220-300

Alisema ununuzi wa ndege hizo ni mkakati muhimu wa serikali inayotekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ni sehemu ya kurahisisha usafirishaji wa mazao ya Kilimo hivyo kuboresha sekta ya Kilimo sambamba na kuinua kipato cha wananchi kwani mazao mengi yanaoza shambani lakini kupitia usafirishaji huo mazao yote yatakuwa na tija.

Jambo la nne ni kuhusu Elimu bure, Waziri Hasunga alisema kuwa Katika kipindi cha muda mrefu Tanzania kulikuwa na wimbi la wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na wazazi/walezi kukosa fedha za kuwalipia ada. Katika kuliona hilo Rais Magufuli aliamua kufuta ada kuanzia elimu ya awali hadi sekondari, jambo ambalo limeongeza idadi ya wanafunzi ambao wamejitokeza kusoma.

Alisema kuwa maono ya Rais Magufuli yamezaa matunda kwani wananchi wengi sasa watoto wao wananufaika na serikali yao kwani imekuwa mkombozi katika sekta ya elimu.

Mikutano hiyo ilifanyika katika Mtaa wa Mantengu A na B na Mtaa wa Old Vwawa kata ya Vwawa, kata na Mtaa wa Ilolo, Mtaa wa Jimu kata ya Ichenjezya, na Mtaa wa Isangu kata ya Hasanga. Kadhalika amefungua shina namba 6 la wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi Mtaa wa Mantengu B pamoja na kukagua mradi wa maji wa Vwawa unaojengwa katika katika eneo la Mantengu.

MWISHO

No comments:

Post a Comment