Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wanunuzi na watumishi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifatilia jinsi mnada wa kahawa unavyoendeshwa mara baada ya uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imewataka wakulima wote nchini kwa kupitia
vyama vya Ushirika kuweka mkakati wa kununua na kutumia mitambo ya kuchakata
kahawa ili kuongeza na kuwa na mwendelezo (Consistency) wa ubora wa kahawa
inayozalishwa ili kupata bei nzuri mnadani au kwenye soko la moja kwa
moja.
Waziri wa Kilimo amesema hayo Leo tarehe 22 Agosti
2019 wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe na kuzitaka
Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya mapato kuendelea kuwekeza katika
uendelezaji wa zao la kahawa ikiwemo uzalishaji wa miche, ununuzi wa CPU na
kuwawezesha wakulima na maafisa ugani kupata mafunzo ya kilimo bora cha kahawa
ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi.
Alisema kuwa ili kulinda ubora wa kahawa, matumizi
ya mitambo ya kisasa ya kuchakata kahawa (CPU) hayawezi kuepukika. Alisema
nchini kuna takribani mitambo 481 kiasi ambacho bado kipo chini ukilinganisha na
kiasi cha kahawa inayozalishwa. "Hivyo nawasihi wadau wote muone umuhimu
wa uwepo wa mitambo hii kwa kuwa ili upate kahawa nyingi zenye sifa za ubora
unaofanana ni lazima kuwepo na matumizi makubwa ya CPU tena kwa kuzingatia
hatua zote za uchakataji wa kahawa" Alikaririwa Mhe Hasunga
Mhe Hasunga aliongeza kuwa Lengo la Serikali ni
kuona kwamba kahawa zote zinaandaliwa katika mitambo ya kisasa (CPU) ili zipate
bei nzuri katika masoko kwani dhamira ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni
kuimarisha tija katika uzalishaji kadhalika kutafuta masoko ya mazao nje na
ndani ya nchi.
Alisema kuwa Ili kuhakikisha tasnia ya kahawa
inaondokana na changamoto ya tija ndogo na uzalishaji, Serikali kwa
kushirikiana na Wadau imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo kuongeza
kasi ya upatikanaji wa miche bora ya kahawa kupitia TACRI; Ruzuku ya miche
inayotolewa na Bodi ya Kahawa na kuanzisha utaratibu wa upatikanaji wa mikopo
ya mbolea kwa wakati kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na
Sekta Binafsi.
Aliongeza kuwa hatua hizo zimewezesha kuongezeka
kwa uzalishaji wa kahawa kutoka tani 43,625 za kahawa safi msimu wa mwaka
2017/2018 mpaka kufikia tani 68,147 msimu 2018/2019.
Waziri huyo wa kilimo Mhe Hasunga alisema kuwa
takwimu zinaonyesha kuwa tija katika uzalishaji wa kahawa kwa wakulima wadogo
wa kahawa ni ndogo sana ukilinganisha na wakulima wa mashamba makubwa na
wakulima wa kahawa wa nchi nyingine.
Aliongeza kuwa Wastani wa tija kwa mti mmoja wa
kahawa ya Arabika ni gramu 350 ikilinganishwa na kilo moja (gramu 1,000) kwa
nzi za Brazil na Vietnam.
Aliziraja Sababu kubwa zinazosabisha tija ndogo
kwenye kahawa kuwa ni pamoja na Matumizi madogo ya mbolea na virutubisho kwa
ajili ya kuongeza tija na uzalishaji; na Wakulima kutokuzingatia kanuni za
kilimo bora cha kahawa ambapo wakulima wengine hawatunzi kabisa miti yao ya
kahawa na huvuna tu kile kitakachopatikana.
Sababu nyingine ni Uwepo wa magonjwa na wadudu
waharibifu wa kahawa Miti iliyozeeka sana na kupoteza uwezo wa kuzaa vizuri;
Badala ya kutumia miti iliyoboreshwa yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa
na kuzaa sana. Nimeambiwa mti wa mmoja ulioboreshwa unao uwezo wa kuzaa wastani
wa kilo 3 – 5 za kahawa kavu (Parchment).
Aidha, Mhe Hasunga amsema kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano imedhamiria kwa dhati kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya kahawa na
kuhakikisha inaendelea kutoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini, kuongeza
pato la taifa na kuongeza ajira kupitia viwanda mbalimbali vya kahawa.
Moja ya lengo kuu la Serikali ya Awamu ya Tano ni
kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Ili kufikia lengo hilo, Serikali
kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha matumizi ya miche
bora ya kahawa ili kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima, kuimarisha
mazingira ya biashara na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya kahawa ili
kuiwezesha kutoa mchango unaohitajika katika kujenga Tanzania ya
viwanda.
Kuanza kwa minada ya kanda ya kahawa ni utekelezaji
wa maagizo ya Serikali kuwa kuanzia msimu wa kahawa 2019/2020 Bodi ya Kahawa
ianze kuendesha minada ya kahawa katika Kanda nne (4) za uzalishaji wa kahawa.
Kanda hizo ambazo minada ya kanda itafanyika ni Kanda ya Mbeya/Songwe mnada
unafanyika Mbozi, Kanda ya Ruvuma/ Njombe mnada unafanyika Mbinga Mkoani
Ruvuma, Kanda ya ziwa mnada unafanyika Bukoba Mkoani Kagera na Kanda ya
Kaskazini mnada unafanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro.
MWISHO
Ok! It's good! We really appreciate the work of the third phase government! Viva President JPM
ReplyDeleteila mimi kwa mtizamo wangu soko huria kama ilivyokuwa miaka ya nyuma mfano 2010 2015 kahawa ilifika hadi 6000 kwa kilo kitu ambacho kiliboresha maisha ya wananchi wengi tofauti na ushirika ambao umeibuka hivi karibuni na bei kushuka mpaka 4000kwa kilo bei ya juu na 3300 kwa bei ya chini hivyo nakubali kwamba walioafiki ushirika hawakufanya utafiti hivyo vijana tuangalie suala hili kwa undani zaidi
ReplyDelete