Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman Jafo akitoa hotuba
wakati wa uzinduzi wa Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania
uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru akitoa neno la utangulizi kabla ya
uzinduzi wa Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania uliofanyika jijini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Anjelina Mabula akitoa neno katika
uzinduzi wa Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania, Dodoma.
Mchumi
Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Rora Madete akitoa neno la
shukrani baada ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania
uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman Jafo, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru na Mchumi Mkuu
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Rora Madete wakifuatilia kwa
karibu maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Utafiti wa Kiuchumi
na Kijamii, Dkt. Tausi Kida katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa
Uendelezaji Miji Tanzania, Dodoma.
Meza kuu wakiongozwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman
Jafo, wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya washiriki hafla ya
uzinduzi wa Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania uliofanyika katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Seleman Jafo akimkabidhi
kitabu cha Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania, Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru baada ya kuzindua
Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania, Dodoma.
******************
Na. Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali
imezindua rasmi Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania ili kuhakikisha
nchi inakuwa na miji iliyopangwa na makazi yenye huduma zote za kijamii
ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka
mitano 2016/17-2020/21.
Mpango huo
umezinduliwa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo, katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mpango kazi huo, Waziri Jafo alisema kuwa Serikali
imejidhatiti kuandaa mipango miji madhubuti ambayo imezingatiwa katika
miongozo ya kuandaa mipango ya taifa.
“Serikali
inazindua rasmi Mpango huo ili kuleta mpangilio mzuri wa Miji wenye
manufaa kwa Taifa na kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye manufaa
ya kiuchumi na kijamii kwa nchi”, alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo
alisema kuwa mpango huo umejikita katika maeneo manne ambayo ni matumizi
ya lugha ya mpango kazi, suala la utawala na kanuni, mkakati wa fedha
pamoja na kuchunguza njia za kukuza uchumi kwa kutambua njia ambazo
zitachochea ukuaji wa uchumi katika viwango vya juu.
Alisema kuwa
maeneo hayo manne ni muhimu kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye
manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kuwa unatoa mapendekezo ya msingi kwa
wakati ambayo ni muhimu kwa upangaji wa maendeleo ya miji nchini.
Kwa upande wake
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.
Angeline Mabula, alisema kuwa ukuaji wa miji ni suala pana ambalo
linahitaji wadau wengi kuunganisha juhudi ili kuhakikisha ukuaji wa miji
inayosimamiwa kikamilifu.
Dkt. Mabula
amesema kuwa, wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano katika kuleta
pamoja jitihada za kila taasisi ili kuepuka jambo moja kufanywa na wadau
zaidi ya mmoja, lengo likiwa kufanikisha malengo ya nchi iliyojiwekea.
Naye Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolph Ndunguru,
aliwashukuru viongozi na wote waliohudhuria katika hafla hiyo muhimu kwa
Taifa na kueleza kuwa mpango huo utasaidia kutatua changamoto za
upangaji miji kwa maendeleo ya uchumi na Taifa kwa ujumla.
Vilevile
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa kiuchumi na Kijamii, Dkt.
Tausi Kida, amesema Mpango huo utasaidia katika uandaaji wa mipango ya
kitaifa ya uendelezaji miji pamoja na uandaaji wa sera kwa kuwa
uliotokana na utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii kwa
kuwa uliofanywa kwa kufuata kanuni za kisayansi za ufanyaji tafiti.
No comments:
Post a Comment