…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
Patrobass Katambi ametahadharisha kwa baadhi ya watu wanaowarubuni na
kuwapatia Mimba watoto wa Shule na kusema kuwa mtu yeyote atakayebainika
amempatia Mimba Mtoto wa Kike hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Mhe.Katambi ameyasema hayo jijini
Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya vijana Duniani ambayo
kwa Tanzania yalianza Agosti 15 na kuhitimishwa Agosti 16 yaliyoenda
sambamba na Bonanza la michezo na Matamasha mbalimbali likikutanisha
zaidi ya Vijana 500 kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema mtu
akimpatia Mimba mtoto wa shule kuanzia chekechea hadi kidato cha sita
atashughulikiwa na kufungwa kwa mujibu wa sheria.
“Kama sheria zilivyo serikali
itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanaowapatia mimba
watoto wa shule,haiwezekani mtoto akose ndoto zake za masomo”amesema
Katambi
Aidha ,Katambi amesema kwa upande
wa wazazi wanaokubaliana ili wayamalize pindi mtoto wa kike anapopatiwa
mimba nao ni wahalifu kama wahalifu wengine na tayari amesema kuna watu
wawili wameshafungwa kutokana na kuwapatia mimba watoto wa shule.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo
wa wilaya amesema Serikali itaendelea kuheshimu kazi kubwa zinazofanywa
na asasi za kimataifa ikiwa ni Pamoja na elimu ya Uzazi ,kuwajali wenye
ulemavu,kuwawezesha kiuchumi na kupinga mimba za utotoni.
Mkuu huyo wa Wilaya ameendelea
kufafanua kuwa zaidi ya Tsh.Bilioni 2.5 na zaidi katika jiji la Dodoma
zimetengwa kwa ajili ya Vijana huku akizungumzia kuanzishwa kwa
hospitali tembezi ili kuweza kuwafikia vijana walio wengi na Zaidi ya
Tsh.Bilioni 2.9 zimetengwa kwa ajili ya hospitali ya Uhuru.
Pia Mhe.Katambi amesema serikali
ipo tayari kuzifutia leseni taasisi ambazo ambazo zimekuwa zikiwezeshwa
kwa lengo la kusaidia vijana lakini hazitimizi matakwa hayo.
Meneja Program ya vijana na
Maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt.Majaliwa Marwa,amesema UNFPA
itaendelea kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya
Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kupinga mimba na
ndoa za utotoni.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa
Baraza la vijana Zanzibar Bw.Makoti amesema kuwa serikali zote mbili
za Muungano,Bara na visiwani zitaendelea kushirikiana katika kutatua
changamoto mbalimbali za vijana.
Kilele cha Maadhimisho ya Vijana
kimataifa yameenda sambamba na Bonanza na Tamasha la vijana ambao
wamejihusisha michezo mbalimbali iliwa ni pamoja na karate,kufukuza
kuku,kuvuta kamba,kutembea na ndimu kwa kutumia kijiko mdomoni na
uimbaji na kaulimbiu mwaka 2019 ni boresha Elimu.
No comments:
Post a Comment