…………………
Na Munir Shemweta, WANMM TABORA
Idadi
kubwa ya Hati za Ardhi takriban12,000 katika Ofisi ya Msajili wa Hati
imemshtua Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula alipofanya ziara Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi
Kanda ya Magharibi.
Mwishoni
mwa wiki Dkt Mabula akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi sambamba na kukagua masijala
ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Tabora alitembelea Ofisi ya
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi kujionea utendaji kazi wa
kanda inayojumuisha mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma.
Akiwa
Ofisi ya Msajili wa Hati, Dkt Mabula alielezwa na Msajili wa Hati wa
Kanda ya Magharibi Julian Ngonyani kuwa ofisi yake ina takriban hati
12,000 ambazo ziko tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa waombaji lakini
wahusika hawajajitokeza kuchukua kwa sababu ambazo hazijulikani.
Naibu
Waziri Dkt Mabula alishangazwa na idadi kubwa ya Hati hizo na
kubainisha kuwa Hati zilizopo Ofisi ya Msajili wa Hati kama
zingechukuliwa basi wahusika wangekuwa na nyaraka zinazoonesha umiliki
halali wa maeneo yao sambamba na hati hizo kuwasaidia katika shughuli za
maendeleo kama vile kukopa pesa katika mabenki mbalimbali.
Alisema,
Halmashauri katika mikoa ya Kanda hiyo ya Magharibi zinapaswa
kuwajibika kwa kuhakikisha waombaji wanapata hati ambapo alizitaka
kuandaa utaratibu maalum utakaowezesha Hati kupelekwa kwenye halmashauri
husika na waombaji kuzichukua.
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, utaratibu huo utawawezesha wananchi kuchukua hati
zao kwa urahisi bila ya usumbufu ambapo hivi sasa waombaji hulazimika
kuzifuata Ofisi ya Kamishna wa Kanda jambo alilolieleza kuwa ni usumbufu
kwani baadhi ya waombaji hulazimika kutembea umbali mrefu hasa kwa
wale wanaokaa maeneo yaliyo mbali na Ofisi ya Kanda.
‘’Halmashauri
inaweza ikandaa utaratibu wa kupelekewa Hati za Ardhi katika maeneo yao
na Ofisi ya Kamishna wa Kanda na jukumu la halmashauri litakuwa
kugharamia pesa ya kujikimu kwa watumishi wa Kanda watakaopeleka hati na
kuzikabidhi kwa waombaji, hiyo itasaidia kuwapunguzia mzigo wananchi’’
alisema Dkt Mabula.
Katika Hatua Nyingine,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameikabidhi Hati ya Kiwanja No 47 Block A Chama cha Mapinduzi wilaya ya
Tabora kilichopo eneo la Kanyenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora baada
ya kiwanja hicho kuwa na mgogoro wa muda mrefu Kati ya ofisi ya CCM na
Shirika la Utangazaji (TBC).
Dkt
Mabula alimkabidhi hati hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya
Tabora Mohamed Katete ambapo makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Katibu
wa CCM mkoa wa Tabora Solomon Kasaba, Katibu UWT mkoa Rehema Mohamed,
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharbi Idrissa Kayera na Msajili
wa Hati wa Kanda Julian Ngonyani.
Katika
Makabidhiano hayo, Dkt Mabula alisema Chama cha Mapinduzi kina maeneo
mengi inayomiliki lakini siyo yote yenye hati na kubainisha kuwa
kukabidhiwa hati hiyo iwe chachu kwa chama kuhakikisha maeneo yake yote
yanakuwa na hati kuepuka migogoro.
Ametoa
wito kwa CCM kuhakikisha maeneo ya Kata yanayomilikiwa na chama hicho
yasiyopimwa yanapimwa na kupatiwa hati na hata yale yasiyo pimwa basi
yawe na mipaka na kubainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutaondoa migogoro
na kukifanya chama kuwa na miliki halali ya maeneo yake.
No comments:
Post a Comment