Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Mwanga, katika
ukumbi wa Green Bird, wilayani hapo, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, wakati
alipowasili kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) na
kuongea na wananchi, katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai
20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akiangalia mashine za kusukumia maji, kwenye mradi wa maji wa Same,
Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu,
Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akiangalia chanzo cha maji, katika mradi wa maji wa Same, Mwanga,
Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai
20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akifafanuliwa jambo na Kiongozi wa Mradi, Richard Magwizi, wakati
akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika
kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. Katikati ni Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika
kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza na wananchi, baada ya kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga,
Korogwe (SMK) katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ulioko Kirya, wilayani
Mwanga, na kukagua hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo.
Waziri Mkuu amekagua ujenzi huo
jana (Jumamosi, Julai 20, 2019) na kutoa maelekezo kadhaa ili
kuharakisha ujenzi wa mradi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu
sasa.
Akizungumza na wakazi wa Kirya,
Nyumba ya Mungu na vijiji vilivyo jirani na eneo la mradi, Waziri Mkuu
alisema Serikali itaendelea kutoa fedha hatua kwa hatua ili kukamilisha
mradi huo.
Waziri Mkuu amewataka wakazi hao
waache kutumia uvuvi haramu na badala yake, wavue samaki kwa kutumia
njia halali. “Bwawa la Nyumba ya Mungu linagusa wilaya tatu za Mwanga,
Simanjiro na Moshi Vijijini. Ninataka Serikali za wilaya husika
zisimamie jambo hilo,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Pauline Nkwama
amsimamie Afisa Elimu wa Wilaya hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi,
Bibi Mariana Mgonja na kuhakikisha kuwa anawahamishia walimu kwenye
shule mbili za Kirya ambazo zilikuwa na walimu wawili wakati zina
wanafunzi zaidi ya 400 kila moja.
“Afisa Elimu Mkoa hakikisha Afisa
Elimu wa elimu ya msingi katika wilaya hii anahamisha walimu kutoka
pale mjini na kuwaleta huku ili huku vijijini kuwe na walimu sita katika
kila shule. Kesho Jumapili (leo) andika barua za uhamisho, Jumatatu
wapewe ili Jumanne waje kuripoti huku,” alisema.
Alimwagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mwanga, Bw. Zephrin Lubuva awatafutie gari walimu
watakaohamishiwa huko ili wafike mapema.
Amechukua hatua hiyo, baada ya
kuelelezwa na mbunge wa jimno hilo, Profesa Jumanne Maghembe kwamba
katika eneo hilo kuna shule mbili ambazo zina walimu wawili wakati kuna
madarasa nane, yaani la awali moja na ya msingi saba, na wanafunzi zaidi
ya 400. Alizitaja shule hizo kuwa ni Kiti cha Mungu na Emangulai.
Mapema, akitoa taarifa kuhusu
mradi huo, msimamizi wa mradi huo Mhandisi Richard Magwizi alimweleza
Waziri Mkuu kwamba Serikali inatekeleza mradi huo ili kuondoa kero ya
maji inayowakabili wakazi wa miji ya Same na Mwanga na vijiji 38 vilivyo
katika eneo la mradi.
Alisema mradi huo
utakapokamilika, unatarajiwa kunufaisha wananchi 438,931 katika Wilaya
za Same (246,793), Mwanga (177,085) na Korogwe (15,053). Alisema mradi
huo umegawanywa katika awamu mbili za utekelezaji na unakadiriwa
kugharimu dola za Marekani milioni 300.
“Awamu ya kwanza inahusisha
ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa maji safi na kusambaza maji kwa
wakazi wa Mji wa Same na Mji wa Mwanga na vijiji 9 vilivyo kandokando ya
chanzo cha maji ambapo awamu ya pili itahusisha ujenzi wa miundombinu
ya usambazaji wa maji katika vijiji 29,” alisema.
Akielezea changamoto
zinazowakabili, Mhandisi huyo alisema wana changamoto ya kuchelewa kwa
malipo ya mkandarasi kutokana na uwiano wa uchangiaji ambapo Serikali
inagharimia asilimia 50.18. “Malipo yanapochelewa, yanaathiri kasi ya
utekelezaji,” alisema.
No comments:
Post a Comment