Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli amemteua
George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira.
Simbachawene anachukua nafasi ya
January Yusuf Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua
Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Bashe anachukua nafasi ya Innocent
Lugha Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli
amemteua Balozi Dkt. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka
ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo
tarehe 21 Julai, 2019.
No comments:
Post a Comment