WAZIRI JENISTA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
akizungumza na waombolezaji wakati alipowaongoza katika Ibada na kuaga
mwili wa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Richard Kalinga, nyumbani kwa
marehemu jijini Dodoma, Julai 22, 2019. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi
wa Idara ya Maadhimisho, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mohammed Kiganja
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Jenista Mhagama akitoa pole kwa familia ya mtumishi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Marehemu Richard Kalinga, baada ya kuwaongoza waombolezaji katika
Ibada ya kumwombea marehemu na kutoa heshima za mwisho, nyumbani kwa
marehemu jijini Dodoma Julai 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment