Na George Binagi, Mwanza
Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tawi la Tanzania, imeandaa
warsha kwa viongozi (wahariri na mameneja) wa vyombo mbalimbali vya habari hapa
nchini ili kuwajengea uwezo kufanya kazi kwa welezi zaidi.
Warsha hiyo
ya siku tano imeanza leo jumatatu Julai 22, 2019 jijini Mwanza lengo kuu likiwa
ni kuimarisha utendaji kazi wa viongozi hao katika kutoa habari linganifu
pamoja na kupata mbinu za jinsi ya kujilinda wakiwa katika mazingira hatarishi
ya kazi.
Mkurugenzi
wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amesema miongoni mwa mada
zitakazowasilishwa kwenye warsha hiyo ni pamoja na umuhimu wa kuripoti habari
linganifu hususani kipindi cha uchaguzi, nafasi ya mwanamke katika vyombo vya
habari na chaguzi mbalimbali.
Gasirigwa amezitaja
mada nyingine kuwa ni jukumu la vyombo vya habari katika kukuza demokrasia,
uandishi unaozingatia maadili, usalama wa waandishi wa habari mtandaoni pamoja
na mazingira hatarishi ya waandishi wa habari.
Washiriki
wamesema warsha hiyo ni muhimu kwao katika kipindi hiki ambacho Tanzania
inaelekea kwenye uchaguzi mdogo mwaka huu 2019 pamoja na uchaguzi mkuu hapo mwakani
2020 na kwamba elimu watakayoipata watahakikisha inawafikia waandishi wa habari
wengine katika vyombo vyao vya habari.
Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania imeshirikiana na
taasisi ya IREX ya nchini Marekani pamoja na Ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania kufanikisha warsha hiyo inayotarajiwa kufikia tamati ijumaa Julai 26,
2019.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akitoa neno la ufunguzi kwenye warsha hiyo inayofanyika Adden Pallace Hotel jijini Mwanza.
Sarah Bushman kutoka taasisi ya IREX akitoa salamu zake kwenye warsha hiyo.
Ben Ellis kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania akisisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia weledi katika utendaji wao wa kazi.
Mshiriki Fredy Herbert kutoka Bomba FM ya jijini Mbeya akiwasilisha maoni ya washiriki wenzake kupitia makundi.
Mhariri kutoka Clouds Media Group, Joyce Shebe akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wamekiri kwamba warsha hii ni muhimu kwao wakati ambao Tanzania inaelekea kwenye chaguzi.
Scolastica Mazula kutoka EFM Radi akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
Wawakilishi kutoka taasisi ya IREX na Ubalozi wa Marekani wakifuatilia warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment