WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE APOKELEWA OFISI NDOGO YA MAKAMU WA RAIS DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.
Mussa Sima (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene
(katikati) katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam
mara baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene akikaribishwa
na Bi. Elizabeth Mtiganzi katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini
Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene akizungumza na
Watendaji na Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani)
katika Ofisi ndogo Dar es Salaam, mara baada ya kuwa kuapishwa Ikulu Dar
es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mhe. Simbachawene amewataka
watendaji hao kushirikiana kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment