Rais Magufuli Atoa Agizo Kero Ucheleweshaiji Vibali NEMC Itatuliwe
Na: Frank Shija – MAELEZO
JPM: Rais John Pombe Magufuli metoa agizo kwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Goerge Simbachawene
kushughulikia kero ya ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji ili
kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.
Amelitaka Baraza la la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC),
kutochelewesha utoaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuongeza ufanisi
katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.
“Pasiwe na ucheleweshwaji wa vibali vya NEMC kwa viwanda vyetu, sisi
tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vikwazo
kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke kwa sababu tunahitaji
viwanda, ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vya NEMC vitafuata
baadae,”alisema Dkt. Magufuli.
Rais Magufuli amemtaka Simbachawene kusimamia kwa karibu suala hilo
la ucheleweshwaji wa vibali vya Tathmini ya uharibifu wa Athari ya
Mazingira vinavyotolewa na NEMC.
Rais Magufuli ameongeza kuwa fedha nyingi zinatolewa na wafadhili
kwa ajili ya miradi ya mazingira lakini kumekuwa hakuna matokeo ya
kuridhisha hivyo ametaka kuwepo usimamizi madhubuti wa rasilimali fedha
inayoelekezwa katika miradi ya mazingira.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amempongeza Naibu Waziri wa
Kilimo, Hussein Mohamed Bashe kwa uchambuzi mzuri wa masuala ya kilimo
aliokuwa anaufanya akiwa bungeni na kuongeza kuwa hiyo ndiyo sababu
ameamua kumteua ili akayatekeleze kwa vitendo kwa ajili ya kukwamua
kilimo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), George Boniphace Simbachawene amesema kuwa shughuli zote za
kiuchumi zinategemea sana mazingira hivyo atashirikiana na wataalamu wa
wa ofisi yake kumshauri vyema Makamu wa Rais katika namna bora ya
kutatua changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira.
Ameongeza kuwa fedha zinazotajwa kuingia katika nchi kwa ajili ya
mazingira ni nyingi lakini zimekuwa zinatumika zaidi katika masuala ya
kiutawala badala ya kuelekezwa katika miradi ya kukabiliana na uharibifu
wa mazingira.
“Nataka nikuhakikishie Mhe. Rais kuwa nitamsaidia Makamu wa Rais
katika Ofisi yake, kwanza natambua lakini pili mimi kwa kushirikiana na
wenzangu nitakaowakuta pamoja na walaalamu nitajitahidi kutoa mawazo
yangu ili tuone ni namna gani tunaokoa mazingira,” alisema Simbachawene.
Akizungumzia masuala ya Muungano, Waziri Simbachawene amesema kuwa
anafahamu kuwa msingi wa Muungano wetu siyo tu yaliyoandikwa katika
Katiba na kufafanuliwa katika sheria bali ni wa kihistoria ambao
unajengeka katika maelewano zaidi badala ya maandishi.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa
anafahamu changamoto zinazowakabili wakulima wa nchi hii hasa
ukizingatia kuwa ndiyo sekta inayowagusa asilimia kati ya 60-70 ya
watanzania wote, wengi wao ndiyo wanyonge ambao Rais Magufuli ndiye
mtetezi wao.
Amesema kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kwa mamlaka atakayopewa
kuhakikisha anamsaidia Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi
ili kukwamua sekta ya Kilimo nchini.
Hafla hii ya uapisho imefanyika kufuatia Mhe. Rais kufanya
mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari
Makamba na nafasi yake kuchukuliwa na Waziri George Simbachawene, huku
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akijaza nafasi iliyoachwa wazi na
Mhe. Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara.
Na: Frank Shija – MAELEZO
Rais John Pombe Magufuli metoa agizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Mhe. Goerge Simbachawene kushughulikia kero ya
ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuendana na kasi ya uchumi
wa viwanda.

No comments:
Post a Comment