Friday, July 12, 2019

TIGO YATANGAZA MSHINDI WA KITITA CHA MILIONI 10 KUPITIA PROMOSHENI YA SOKA LA AFRIKA

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kumtangaza mshindi wa mwezi wa shilingi milioni 10/, kupitia promosheni ya SOKA la AFRIKA , Omary Ahmed Bwenda, (Kulia) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi na kukabidhiwa fedha zake.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10/- Omary Ahmed Bwenda (27 (kulia) mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, kutokana na kuibuka mshindi kupitia promosheni inayoendelea ya Tigo inayojulikana kama SOKA la AFRIKA katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, baada ya kufanikisha ndoto za wateja wake 10 kushuhudia mashindano ya soka ya Afrika, mubashara kupitia promosheni yake ya SOKA la AFRIKA, imetangaza mshindi wa fedha taslimu shilingi milioni 10 kupitia promosheni hiyo. Akiongea katika mkutano na waandishi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, alimtangaza mshindi huyo wa mwezi kuwa ni Omar Ahmed Bwenda (27) mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es Salaam. Amesema kupitia promosheni hii iliyoandaliwa na Tigo kwa ajili ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuiunga mkono kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zake imewawezesha pia wateja 28 kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila siku na wateja wanne kujishindia milioni 1,000,000/- kwa mwezi. Kupitia promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu washiriki wataendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kila siku, kwa wiki na kwa mwezi. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15670 au tembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz na kujibu maswali kuhusiana na michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri. “Natoa wito kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kuendelea kuchangamkia na kushiriki promosheni hii ya SOKA la AFRIKA ili waweze kujishindia zawadi, na kadri wanatavyoshiriki na kujibu maswali ndivyo watakavyokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata ushindi” alisema Shisael, na kuongeza kuwa na kuongeza kusema kuwa hadi kufikia mwisho wa promosheni hii, zaidi ya wateja 100 watajishindia zawadi ya pesa taslimu. Mashindano ya promosheni ya SOKA LA AFRICA ni sehemu ya jitihada za Kampuni ya Tigo, kuwashukuru wateja wake kwa kutumia bidhaa na huduma za Kampuni. Pia promosheni hii ni sehemu ya ubunifu ambao umelenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wateja.

No comments:

Post a Comment