Mhe. Eng. Stella Manyanya (Mb.) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Pamoja na Mhe. Marjolin Sonnema Naibu Waziri wa Kilimo na
Ubora wa Chakula kutoka nchini Uholanzi pamoja na delegation yake wakiwa katika
majadiliano ya pande mbili (bilateral meeting) kujadili ushirikiano wa
kibiashara baina ya nchi hizi mbili kwa faida ya pande zote walipokutana Arusha
tarehe 10/7/2019.
Mhe. Eng. Stella M. Manyanya (Mb.) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akizungumza na
washiriki wa Semina ya "Ubia wa Tanzania na Uholanzi katika Biashara
Endelevu" jijini Arusha , pamoja na mambo Mengine
aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kuwezesha miradi mbalimbali ya kilimo na
ufugaji biashara nchini na kuomba miradi hiyo ienee zaidi hasa vijijini ili
kukuza kilimo kwa mustakabali wa uendelezaji Viwanda. Pia, Naibu waziri alieleza
jitihada za Serikali za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo
utekelezaji wa Blueprint.
Kutoka kulia ni Mhe. Abdallah Ulega Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Mhe.naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Manyanya, Mhe. Sonnema ambaye ni Naibu waziri wa kilimo-Uholanzi, Mhe. Anna Mgwira RC
Kilimanjaro na Mhe. Jeroen Verheul Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania
wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya miradi mbalimbali katika Semina ya Ubia
wa Tanzania na Uholanzi ktk Biashara Endelevu jijini Arusha, tarehe
10/7/19
No comments:
Post a Comment