Monday, July 22, 2019

HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA DODOMA YATOA TAMKO KUHUSU WARAKA WA MAKATIBU WAKUU WASTAAFU





Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Bw.Henry Msunga ,akiwasilisha taarifa ya tamko la Halmshauri kUU ya CCM Mkoa wa Dodoma ikilaani vikali waraka wa makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dodoma ndugu Godwin Mkanwa,akizungumza mara baada ya kutoa taarifa juu ya kulaani vikali waraka wa makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho.

Sehemu ya wananchama wa CCM Mkoa wa Dodoma wakifatilia taarifa ya kulaani vikali waraka wa makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho.

 ........................................

NA  FRED ALFRED

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imelaani vikali waraka wa Makatibu Wakuu wastaafu wa chama hicho walioutoa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni bila ya kufuata Kanuni na taratibu zilizopo.

Akiwasilisha tamko hilo leo jijini Dodoma Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa Henry Msunga  amesema kitendo hicho cha kumhusisha mwanaharakati Cyprian Musiba  na CCM ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na miiko ya chama.
Amesema matamko yaliyotolewa na Musiba ni ya binafsi na hivyo ilipaswa viongozi hao wastaafu kushughulika na mtu binafsi na sio taasisi

“kitendo cha kumuhusisha mwanaharakati cypriani musiba na chama chama cha mapinduzi ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na miiko yay a chama hasa ikizingatiwa kwamba matamko yaliyotolewa ni ya binafsi hivyo ilipaswa viongozi hawa washughulike na mtu na sio chama”alisema
.

Mbali na hayo amesema halmashauri Kuu ya CCM mkoa inaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kazi nzuri inayoifanya.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa ndugu Godwin Mkanwa amesema CCM mkoa wa Dodoma ipo imara na  imejipanga kuhakikisha inatetea haki za wanyonge.

“sisi tupo tayari kushirikiana na mh raisi kwa kazi nzuri anazozifanya za kutetea haki za wanyonge  na kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 kila mkazi wa Dodoma anakua na makazi mazuri hiyo inaonyesha jinsi gani chama kinafanya kazi”alisema mkanwa

No comments:

Post a Comment