…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali ya Ujerumani imetoa Euro milioni 6.0 kwa ajili ya kusaidia
miradi ya maji nchini ikiwemo kuboresha usambazaji na miundombinu ya maji.
Makubaliano hayo yalisainiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo na Mkuu wa Programu ya
Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) Dr. Johannes
Schoeneberger
Akizungumza katika makabidhiano hayo,
Profesa Mkumbo aliwataka watumishi wa wizara hiyo kutekeleza yale
yaliyomo katika makabiliano hayo bila visingizio.
“Serikali hii ni Serikali ya matokeo sio
mchakato. Kama kununua magari basi tununue magari sio stori ndefu unajua
tulishatoa tangazo sijui limeenda wapi tunataka matokeo,”amesema
Prof.Mkumbo
Kwa upande wake Dr. Johannes
Schoeneberger alisema kuwa fedha hizo si fedha za Serikali ya Ujerumani
bali ni fedha za walipakodi wa Ujerumani na hivyo zitumike kuwasaidia
walengwa ambao ni Watanzania.
“Matumizi, matokeo, utendaji, uhakikishaji yazingatie kuwa ni
ushirikiano huu unalenga katika kumfikia mwananchi kupitia Wizara
No comments:
Post a Comment