Friday, July 12, 2019

JAFO KUKUTANA NA WALIMU WA KILA SOMO KWA WANAFUNZI WALIOTINGA 10 BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amepanga kukutana wa walimu wote wa masomo kutoka shule za Serikali ambazo zinasimamiwa wa TAMISEMI ambao wanafunzi wao waliingia katika nafasi 10 bora katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa

 Pamoja na walimu hao, Pia Waziri Jafo atakutana na wakuu wa shule 64 za Serikali zilizoingia katika shule 100 bora hapa nchini.

Hii itakuwa ni faraja kubwa kwa walimu hao kukutana na Waziri wao kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.

No comments:

Post a Comment