JESHI LA POLISI DODOMA LAFANYA MSAKO NA KUKAMATA MAWAKALA HEWA 47 ,LAINI ZA SIMU 4667
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa
Kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] kwa kanda ya
kati limefanya Operesheni Maalum ya kuwasaka watu wanaojihusisha na
usajili wa laini za simu bila idhini ya makampuni husika ya Simu na
kukamata mawakala hewa 47 na laini za simu 4667..
Akizungumza na Waandishi wa Habari
jijini Dodoma , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gillese Muroto amesema
katika Msako huo umehusisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma
yakiwemo Majengo,Sabasaba,Mipango,Nyerere Square,Sokoni,St.John ,
Chang,ombe ,Nanenane, na Nkuhungu,Bahi ambapo wamekamata wanaume 38 na
wanawake 9 jumla yake 47.
Kamanda Muroto amesema katika Msako huo
wamekamata vielelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na laini za simu
ambapo Vodacom 1300,tigo 1808,Airtel 716 ,Hallotel 694,TTCL 144 ikiwa
ni jumla ya laini 4667 pamoja na simu 50 zilizokuwa zikitumika katika
usajili huku pia jeshi hilo likibaini makosa ya kitambulisho kimoja
kutumika kusajili laini zaidi ya Mtu mmoja ambapo ni makosa kisheria.
Hata hivyo,Kamanda Muroto ametoa wito kwa
Waandishi wa Habari kuendelea kuelimisha jamii juu ya Masuala ya
usajili ili wananchi waweze kuelewa juu ya mawakala matapeli wanaoweza
kuiba nyaraka na taarifa muhimu za mawasiliano na utambuzi ikiwani
pamoja na vitambulisho.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania[TCRA]kanda ya kati amelishukuru jeshi hilo kwa
ushirikiano huku akitoa wito kwa makampuni ya simu husika kukaa makini
juu ya usajili wa laini za simu katika kupambana na wahalifu.
Msako huo ulilenga kukamata Mawakala
wasio kuwa na barua rasmi kutoka kampuni husika ya simu,msajili
alisiyekuwa na ofisi anuani na makazi ya Kudumu,asiyekuwa na leseni ya
biashara au vitambulisho vya biashara vilivyotolewa na Rais John Pombe
Magufuli.
No comments:
Post a Comment