SERIKALI SASA KUANZA KUTOA HATI ZA ARDHI MIKOANI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wiliam Lukuvi akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo,
wataalamu wa ardhi, makatibu Tawala wa mikoa na wakurugenzi wa
Halmashauri wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano huo uliokuwa na lengo la kutathmini na kuweka malengo ya wizara
hiyo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika, akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mkutano huo uliokuwa na lengo la kutathmini na kuweka malengo ya
wizara hiyo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais,
Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhandisi Joseph
Nyamuhanga, akizungumza katika mkutano huo, alipokuwa akitoa salamu za
wizara yake.
Mkuu wa Wilaya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza, akizungumza alipokuwa akitoa salamu za mkoa, wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
wakifuatilia kwa makini mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa ardhi,
na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi waliokutana kutathmini namna
ya kuiendeleza sekta hiyo ili kufikia malengo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Wiliamu Lukuvi, wanne kutoka kushoto waliokaa, na wa tatu kushoto
Naibu waziri wa Wizara hiyo, Dkt Angelina Mabula, wakiwa katika picha
ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya kumalizika kwa
ufunguzi wa mkutano huo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Wiliamu Lukuvi, wanne kutoka kushoto waliokaa, na wa tatu kushoto
Naibu waziri wa Wizara hiyo, Dkt Angelina Mabula, wakiwa katika picha
ya pamoja na Wakuu wa Idara na wataalamu wa Ardhi kutoka mikoa
mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mkutano huo.
…………………………………
Na.Alex Mathias,Dodom
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wiliam Lukuvi, amesema serikali itaanza kusajili nyaraka na hati
milki za ardhi ndani ya mkoa husika, badala ya utaratibu wa mwanzo wa
kusajiliwa ndani ya kanda zilizokuwa zimetengwa lengo ni kupunguza
ucheleweshaji wa usajili wa nyaraka hizo na kuepusha usumbufu wa
wananchi.
Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo leo
Jijini Dodoma wakati akifungua, mkutano wa wataalamu wa sekta ya ardhi
na wakurugenzi na makatibu tawala wa mikoa, wanaokutana jijini Dodoma,
kutathmini malengo ya sekta hiyo, sambamba na kuwajengea uwezo
wataalamu hao namna bora ya ufanyaji kazi na namna ya kutatua
changamoto zilizopo.
Amesema wamekusudia kuhamisha ofisi za
kusajili nyaraka za ardhi kutoka katika kanda, na kuzirudisha ndani ya
mikoa husika, ili kurahisisha zoezi hilo, na upatikanaji wa nyaraka hizo
kwa wakati, na tayari wakuu wa mikoa wameridhia na kutoa majengo
yatakayotumika kama ofisi za wizara za usajili ndani ya mikoa.
“Nataka hatimiliki zote zitolewe na
kusajiliwa mikoani kwani watu wamekuwa wakipoteza muda na gharama nyingi
za usafiriki kufuatilia hati hivyo hatuwatendei haki hawa wananchi
wanyonge kwa kuwatwisha mzigo wa gharama”amesema Lukuvi.
Na katika kuhakikisha wananchi wanyonge
wanapata huduma stahiki, amepiga marufuku wakuu wa idara za ardhi
kupokea tozo ambazo hazistahili, pamoja na utumiaji wa madalali ndani ya
ofisi za umma.
Amesema kuwa wananchi hivi sasa wamekuwa
wakipatashida kupata hatimiliki zao za maeneo kutokana ofisi nyingi
kuwepo katika maeneo ya kanda pekee yake.
Pia amesema yupo mbioni kuandaa kanzi
data ya matapeli wa ardhi na kuiweka katika tuvuti ya wizara ya ardhi
ili wananchi wawajue na kujiepusha nao ili wasitapeliwe ardhi zao na
watu hao na hata muogopa mtu yeyote.
Waziri Lukuvi pia amesema kuwa haitakuwa
na maana kwa serikali kama itaendelea kuwapa mzigo wa gharama wanachi
wake wakati wa ufuatiliaji wa hati miliki za maeneo yao na ndio maana
wakaja na mpango huu.
“Tunataka kuwasaidia wananchi kupata hati
miliki za maeneo yao huku gharama wanazozitumia ni nyingi leo hii
unakuta mtu anatoka Kigoma anakuja Tabora, kufuata hati lakini tofauti
na nauli anatumia siku saba hadi kumi kukamilisha zoezi hilo”, amesema
Mbali na hilo amewaonya watumishi wa
idara za ardhi nchini kuacha tabia ya kupandisha bei ya maeneo pamoja na
gharama za upimaji kwa madai kuwa wanajiongezea mapato ya ndani.
Amesema bei ya viwanja lazima ziwe
kwamujibu wa sheria zilizowekwa na siyo kila mtu kujipangia bei zake
ambazo zinageuka kuwa kero kwa wananchi na kubaki kumilikiwa na wachache
wenye uwezo wa kifedha.
Amemtaka katibu mkuu wa wizara hiyo
Doroth Wanyika, kuhakikisha anapanga safu ya wakuu wa idara haraka
watakao kwenda kufanya kazi katika ofisi za wilaya na ofisi za mipango
miji na orodha hiyo ipite mikononi mwake kabla ya wahusika kupewa barua
za uteuzi.
Vilevile amesema wataanza kutumia tehama
katika kurasimisha ardhi na wameanza katika mkoa wa Dar es saalam na
unafanya kazi kwa kasi sana na kuanzia mwakani zoezi hilo litakuwa la
Tanzania nzima.
Amebainisha kuwa baada ya mkutano huo
wataanza utaratibu wa kuwapisha kiapo cha maadili kwa watumishi wote
kuanzia ngazi ya wizara hadi ngazi za chini ili kuhakikisha kila mtu
katika kitengo chake anafanya kazi kwa uadilifu mkubwa kuleta
mabadiliko chanya ndani ya wizara hiyo.
Katibu mkuu wa wizara ya Ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi, Doroth Mwanyika amesema kuwa lengo la kikao hicho
ni kufahamiana na kuleta mapinduzi katika sekta ya ardhi nchini.
Amesema lengo jingine ni kupunguza
migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikisababisha kudolola kwa shughuli za
uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la kiwanja kimoja
kumilikishwa kwa mtu zaidi ya mmoja.
kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mabadiliko katika sekta ya ardhi kwa maendeleo ya taifa letu”.
No comments:
Post a Comment