KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI KUJADILI NAMNA BORA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA MWAKA 2019 – 2020
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akizungumza na
Wakurungenzi wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo walipokutana
kujadili maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango kazi wa
mwaka wa fedha 2019 – 2020.
Mkurungenzi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji
Ujuzi Bw. Ally Msaki akielezea jambo kuhusu uwasilishwaji wa mpango kazi
kwa kila taasisi wakati wa kikao kilichowakutanisha kujadili maeneo ya
ushirikiano yanayoitaji utekelezaji wa pamoja.
Baadhi ya Wakurugenzi wakifuatilia kwa
makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa kikao
hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la PSSSF, Jijini
Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba.
Sehemu ya wataalamu wa mipango na bajeti
kutoka kwenye taasisi wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe
(hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakisikiliza
maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani), wakati wa kikao
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Bw. William Urio akielezea jambo wakati wa kikao
kilichowakutanisha kujadili maeneo ya ushirikiano yanayoitaji
utekelezaji wa pamoja.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na
Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akiwasilisha taarifa
ya malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo kwa
mwaka 2019 – 2020.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akipitia taarifa ya
malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi ya OSHA kwa
mwaka 2019 – 2020, wakati wa kikao kilichowakutanisha kujadili na
kukubaliana maeneo ya ushirikiano.
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Bezil Ewala akiwasilisha taarifa ya
malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo kwa
mwaka 2019 – 2020, wakati wa kikao hicho.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO
OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………
NA; MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe amekutana na
Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa lengo la
kujadili kwa kina maeneo watakayo shirikiana kwa pamoja katika mpango
kazi wa mwaka 2019 – 2020 na kutoa maelekezo juu ya namna bora ya
kuhudumia wananchi kulingana na huduma zinazotolewa na taasisi hizo.
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho
kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini
Dodoma, alisema kuwa Mwaka wa fedha 2019/2020 ni muhimu kukubaliana kwa
pamoja maeneo ambayo yatatekelezwa kwa ushirikiano ili kuimarisha
utendaji wa shughuli mbalimbali.
“Lengo kuu la kukutana kwetu hapa ni
kuangalia utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwenye mpango kazi wa
kila Taasisi katika mwaka huu wa fedha, na kubaini namna bora ya
kutekeleza maeneo hayo kwa ufanisi,” alisema Massawe.
Katibu Mkuu aliongeza kuwa kupanga na
kukubaliana maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa mpango kazi
kutasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kazi na majukumu ya kila
siku.
“Ninapenda kuona tunakuwa mfano wa
kuingwa kwa kujijengea mwenendo mzuri wa kushirikiana katika utendaji
ili kufanikisha shughuli nyingi kwa wakati mmoja,” alisisitiza Massawe
Aidha, alitoa wito kwa wakuu hao
kuzingatia suala la mawasiliano na uhusianao kwa wadau na wateja
wanaowahudumia ikiwemo kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa kwa wakati.
Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda
alieleza kuwa ushirikiano na taasisi nyingine na wizara ni fursa pekee
itakayo wawezesha kutekeleza dhamira na mikakati waliyopanga ili kuleta
maendeleo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema kuwa yapo maeneo mengi
ya kushirikiana kwa pamoja na mpango kazi wa mwaka ni sehemu ya
utekelezaji wa maazimio yatakayo wasaidia kuwa na ushirikiano endelevu
katika maeneo mbalimbali.
Kikao hicho kiliudhuriwa na Wakurugenzi
na Wataalamu wa Mipango na Bajeti kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala
Pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
No comments:
Post a Comment