RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA PAMOJA NA MELI YA MV BUTIAMA KATIKA ENEO LA BANDARI YA MWANZA SOUTH
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tuta la Sehemu inapojengwa
Chelezo kubwa yenye uzito wa Tani 4000 kwa ajili ya Ujenzi wa Meli mpya
kubwa na ya kisasa itakayohudumu katika Ziwa Victoria kutoka Mwanza
kwenda Bukoba, Kisumu(Kenya) na Jinja nchini Uganda.
Meli ya MV Victoria inayotoa huduma
katika Ziwa Victoria ikiwa katika ukarabati mkubwa. Ukarabati huo
unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa tatu na Mashine Engine zake mpya
zinatarajiwa kuwasili hivi karibuni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo katika eneo la tuta
la ujenzi wa Chelezo ya kujengea Meli hio kubwa na ya kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Meli ya MV Victoria ambayo
inafanyiwa ukarabati mkubwa katika eneo la Bandari ya Mwanza South.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa
Bandari ya Mwanza pamoja na Wabeba mizigo Makuli kuhusu ujenzi wa Meli
hizo. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment