Monday, July 15, 2019

MBOZI MBIONI KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bw. John Palingo akipewa maelezo na Meneja wa RUWASA Mbozi Mhandisi Stephen Mkalimoto-Sengayave akikagua tanki la maji la Itaka lililokarabatiwa hivi karibuni.

Kaimu mkurugenzi Mtendaji Mbozi Bi Halima Mpita akionyesha uso wenye tabasamu baada ya kushuhudia kasi ya ujenzi wa mradi wa maji Itaka unaolenga” kumtua mama ndoo kichwani” kwa vijiji vitano vya  kata za Bara, Itaka na Halungu.

Timu ya wataalamu wa Halmashauri wakiwa pamoja na Katibu Tawala wilaya ya Mbozi Bi Tusubileghe Benjamin (aliyepo katikati)  wakipewa maelezo na Mkandarasi wa mradi huo Bw. Hezron Mwakyembe (kushoto) kwenye eneo la Chanzo cha Maji kinachojengwa Itaka.

Watoto wakiwa kwenye chanzo hcho kuchota maji, mradi huu utakapokamilika utapunguza muda wa kusafiri hadi kwenye chanzo kuchota maji na badala yake watachota ndani ya mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

…………………….

Na Danny Tweve Mbozi

Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo, amesema kukamilika kwa mradi wa maji wa Itaka kutasaidia “kumtua mama ndoo kichwani” kwenye eneo kubwa la tarafa hiyo ambalo kwa kipindi kirefu huduma ya maji imekuwa changamoto kwao.

Akizungumza mara baada ya kukagua tanki la maji la Itaka ambalo ukarabati wake umekamilika  hivyo kuongezeka idadi yake hadi kufikia  matanki matatu  kwenye mradi wa Maji wa Itewe-Itaka, Mkuu huyo wa wilaya amesema mradi huo ni moja ya miradi ya kimkakati itakayowawezesha  wananchi wapatao 12,000 kwa vijiji vya Itaka, Bara, Sasenga na Itewe.

Tenki la maji lililokarabatiwa lina uwezo wa kutunza lita 70,000 hivyo kuwepo jumla ya matenki matenki matatu yatakayotumika kuhifadhi maji moja lenye ukubwa wa lita 100,000 likiwa limejengwa kwenye chanzo cha maji ili kupunguza matumizi ya umeme kwa kuyahifadhi kabla ya kuyasambaza.

Katika ukaguzi wao Mkurugenzi mtendaji wilaya Mbozi Bi Halima Mpita aliyeongozana na Katibu Tawala wilaya ya Mbozi Tusubileghe Benjamin wameelezea kuridhishwa na kasi ya Mkandarasi na kumtaka akamilishe kwa wakati mradi huo ili jitihada za serikali kuleta fedha kwenye miradi hiyo zionyeshe matunda ya kutua mama ndoo kichwani.

No comments:

Post a Comment