RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA ABIRIA WA KIVUKO KATIKA ENEO LA BUSISI SENGEREMA MKOANI MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mwanza
mjini mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Abiria wa Kivuko cha
MV Mwanza na MV Misungwi kuhusu ujenzi wa Daraja litakalopita ziwani
katika eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Mkandarasi wa Daraja
hilo anatarajiwa kupatikana ndani ya miezi miwili na Daraja hilo
litakuwa na urefu wa kilometa tatu zitakazopita majini. Daraja hilo
litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono abiria wa Kivuko
cha MV Mwanza na MV Misungwi mara baada ya kuzungumza nao katika eneo la
Busisi Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kupanda Kivuko cha MV
Mwanza katika eneo la Busisi wakati akitokea Geita. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment