MAMENEJA UNGANISHENI WATEJA KWA SH 27,000 VIJIJI
Moja ya nyumba zilizowashwa umeme na
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu katika kijiji cha Mkindo Wilayani
Kaliua mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(
mwenye kilemba) alizungumza na vijana wanaofanya kazi ya useremala kwa
kutumia umeme wa jua katika kijiji cha Mgambo wilayani Sikonge, Naibu
Waziri alifika kijijini hapo kutembelea kampuni ya uwekezaji
inayozalisha umeme jua na kuwauzia wananchi.
Wakazi wa kijiji cha Wema mwenye ulemvu
wakikabidhiwa kifaa cha umeme tayari ( UMETA) kutoka kwa Naibu Waziri wa
Nishati , Subira Mgalu, aliyekuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya
utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini wilayani Sikonge,
mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(
katikati) akipata maeneo ya namna ya mtambo wa kuzalisha umeme jua
unavyofanya kazi katika kijiji cha Mgambo, Mkola na Mwenge wilayani
Sikonge mkoani Tabora.
Naibu Waziri Subira Mgalu( mwenye
kilemba) na viongozi wengine wakikata utepe kuashirika kuwasha umeme
katika moja ya taasisi za dini katika kijiji cha Mkindo wilayani Kaliua,
mkoani Tabora.
Ujenzi ukiendelea katika kituo cha kupokea na kupoza umeme katika kijiji cha Uhuru, wilayani Urambo mkoani Tabora.
…………………..
Na Zuena Msuya, Tabora
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
amesema mameneja wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) waongeze idadi ya
wateja kwa kuwaunganishia huduma ya umeme wananchi waliopo vijijini kwa
bei ya shilingi 27,000.
Hatua hiyo ni kigezo cha kupima utendaji kazi wa mameneja hayo katika Kanda,Mikoa pamoja na Wilaya mbalimbali nchini.
Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti,
wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa
Umeme Vijijini,( REA) katika Wilaya za Ulyankhulu, Kaliua, Urambo pamoja
na Sikonge Mkoani Tabora, Julai 18,2019.
Katika Wilaya hizo, Mgalu aliwasha Umeme
katika makazi ya watu, Nyumba za ibada,taasisi za umma, visima vya maji
pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hayo.
Akiwa katika wilaya hizo, Mgalu aliwasha
umeme katika kijiji cha Limbula na Kasunga wilayani ni Kaliua, vilevile
katika kijiji cha Mfindo wilayani Ulyankhulu.
Aidha akiwa katika wilaya Urambo aliwasha
umeme katika kijiji cha Wema, pia aliwsha umeme katika kijiji Kikungu
wilayani Sikonge na kuzungumza na wananchi.
Alisema Mameneja wa maeneo husika ndiyo
wenye dhamana kubwa ya kuwafuata wateja katika makazi na kuwashawishi
kuunganishwa na Umeme badala ya kukaa Ofisini na kusubiri wateja.
“Mradi wa REA umekwisha viunganisha na
kuwasha umeme katika vijiji vingi vya Wilaya mbalimbali, naawaagiza
mameneja kufanya kazi ya kuwafuata wananchi huko walipo mkawape elimu
ili muwaunganishe na Umeme, kwa bei ya shilingi 27,000, tunataka kuona
idadi ya watumiaji Umeme inaongezeka”, Alisema Mgalu.
Tangu mradi wa REA umeanza tayari zaidi ya wateja laki tisa(900,000) wameungamishwa na umeme na bado zoezi hilo linaendelea.
Katika ziara yake hiyo, Mgalu alikagua
ujenzi wa kituo cha kupokea na kuponza umeme kilichopo katika kijiji cha
Uhuru wilayani Urambo ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa
ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho inayoendelea.
Sambamba na hilo, alikagua eneo ambalo
litajengwa kituo kingine cha kupokea na kupoza umeme katika kijiji cha
Ipole wilayani Sikonge, ambacho kinatarajia kuanza kujengwa hivi
karibuni.
Vituo hivyo vinajengwa mahsusi kwa lengo
la kuimarisha upatikani wa umeme mwing na wakutosha katika Mikoa ya
Tabora, Kigoma na pamoja na Katavi,pia mikoa hiyo nayo iunganishwe na
gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme unaotokana na mafuta mazito.
Katika hatua nyingine alitembelea kagua
kampuni ya Power Corner katika kijiji cha mgambo wilayani Sikonge,
inayofanya kazi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua na kuwauzia
wakazi wa kijiji cha Mgambo, Mwenge pamoja na Mkola.
Kituo hicho kilipata zabuni ya zaidi ya
shilingi milioni 500 kutoka kwa Wakala wa Nishati Vijiji (REA) kwa lengo
la kuchangia utekelezaji wa kituo hicho ikiwa ni kutekeleza azma ya
serikali kuwainua wazalishaji wadogo wa umeme.
Naibu waziri aliwaagiza watendaji wa
kituo hicho kutoa huduma bora zinazoendana na ghara wanazolipia wananchi
ili mradi huo uwanufaishe wananchi na si kuwakandamiza.
No comments:
Post a Comment