Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Msingi cha cha
Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga akiwa katika ziara ya
siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao hilo,
Julai 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kasism Majaliwa
akipata maelezo kutoka kwa Katibu na Meneja wa Chama cha Msingi cha
Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga kuhusu pamba
iliyokusanywa na wakulima kwenye ghala la ushirika huo, Julai 15, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mikokoteni iliyosheheni pamba wakati alipotembelea ghala la
Chama cha Msingi cha Ushirika cha kijiji cha Mwabakima wilayani Igunga
alikofanya ziara ya siku moja ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao
hilo, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa
pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
Wananchi wa kijiji cha Mwabakima
wilayani Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipowahutubia akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua
mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwabakima wilayani
Igunga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua mwenendo
wa ununuzi wa zao la pamba, Julai 15, 2019. Kushoto ni Waziri wa
Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey
Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment