Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Morogoro
KATIBU mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amefanya ziara
katika Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga-ERPP)
unaotekelezwa katika Wilaya za Kilosa, Kilombero na Mvomero Mkoani Morogoro na
kutorishwa na kasi ya wakandarasi katika ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia
Mpunga.
Mradi wa ERPP unatekelezwa na Wizara ya Kilimo ukiwa na lengo la kuongeza
tija katika uzalisha wa zao la Mpunga kwa kutoa mbegu bora za zao hilo, ukarabati
wa skimu za umwagiliaji ujenzi wa Maghala pamoja na utafutaji wa masoko.
Aidha Mradi wa ERPP unatekelezwa katika Visiwa vya Zanzibar huku
Tanzania Bara ukitekelezwa katika Maeneo matano ya Mkoa huo.
Akiwa katika ziara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe
ametembelea ujenzi wa Maghala katika Kijiji cha Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya
Kilosa, ghala la Kijiji cha Msolo ujamaa Kilombero, Kijiji cha Njage Kilombero
pamoja maghala ya Kijiji cha Kigugu na Mbogo katika Halmashauri ya Wilaya
Mvomero.
Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa serikali haitosita kuwachukulia hatua
wakandarasi hao kwa kuchewesha kazi wanazopatiwa pasina kuwa na sababu za
msingi.
Amesema kuwa hatua zitakazochuliwa ni pamoja kupeleka mapendekezo katika
bodi za wakandarasi ili kampuni hizo ziweze kufutiwa usajili nchini kutokana na
kutotimiza matakwa ya serikali katika ujenzi wa maghala hayo ikiwemo
kutokukabidhi kazi kwa wakati pamoja na ujenzi chini ya Kiwango.
Akiwa katika Kijiji cha Mbogo Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo
ametaka kuchunguzwa kwa Mkandarasi wa kampuni ya Skemu ya Mkoani Morogoro
kutokana kuwa nyuma ya kazi tofauti na Mkataba wa kazi hiyo unavyoelekeza.
Amesema kuwa Mkandarasi huyo pia ameshindwa kuweka uzio mzuri katika
eneo la ujenzi kutokana kutumia mabati mabovu hivyo kumtaka aubomoe kisha
kujenga mwingine kama alivyoekezwa katika mkataba.
Awali Viongozi wanaosimami mradi huo katika Mkoa wa Morogoro
walimueleza katibu Mkuu wa Kilimo kuwa Baadhi wa wakandarasi wamekuwa wazito
katika ujenzi hali inayotia wasiwasi wa kushindwa kukabidhi kazi kwa wakati.
Nao Baadhi ya wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti wameishukuru
serikali kwa kuwaletea mradi huo na kueleza kuwa utakuwa chachu ya kuongeza uzalisha
wa zao la Mpunga hali itakayofanya waweze kuongeza pato lao pamoja na kuchangia
uchumi wa Taifa
kwa Upande wao wakandarasi hao wamesema kuwa awali walikuwa wakikabiliwa
na changamoto mbalimbali huku pia wakimuahidi katibu Mkuu huyo kukamilisha kazi
kwa wakati na kiwango kinachotakiwa na serikali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment