Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti
ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na
wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika
yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa
wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya
menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti
ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na
wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika
yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa
wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya
menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti
ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (Wa pili kulia),
kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Menejimenti ya Maafa Zanzibar,
Makame Khatib Makame, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Benki ya Dunia Tanzania, Edward Anderson na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara
ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Utafiti na Mipango),
Bashiru Taratibu, , wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa
utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa
taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika
katika menejimenti za maafa , mjini Arusha.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya
menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa
ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana
wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa
Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi
hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya
Dunia.
***************
Benki ya Dunia, kwa kushirikiana
na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya
Menejimenti ya Maafa, imeendesha mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya
kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa
Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, kwa wataalamu wa
menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na Idara za serikali
pamoja na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo
hayo, jijini Arusha leo tarhe 19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya
Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa na wataalam wa
kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye
kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na
maendeleo.
“Mafunzo haya yatatusaidia
kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa kuwa na mfumo wa
pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika kuendesha
shughuli ya Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu
binafsi, Taifa na Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza
kuwa na mpango wa pamoja wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.
Matamwe ameendelea kufafanua kuwa
kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa
kurejesha hali, utaalamu huo utaisaidia nchi yetu Tanzania kuwa na
Takwimu za urejeshaji hali ambazo tutapata uwezo wa kurejesha hali
itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.
Akiongea katika mafunzo hayo kwa
niaba ya Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania,
Mtaalamu wa Mawasiliano Benki ya Dunia Edward Anderson amefafanua kuwa
Benki hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na
wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa wakati baada ya maafa
kutokea.
“Tangu mwaka 2016 nilipofika hapa
nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea ikiwemo tetemeko la ardhi
mkoani Kagera, na mafuriko katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016,
hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na Mpango bora katika kurejesha
hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo tayari katika kutekeleza
hayo” Amesema Edward.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo
kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika
kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa
kurejesha hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji,
mbinu za kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji
hali, kuainisha hasara na athari zitokanazo na maafa .
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa
muda wa siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, 2019,
liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa , kwa
wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na
Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali,
limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,
kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
No comments:
Post a Comment