*************
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo ya
hospitali mpya inayojengwa wilayani Itilima Mkoani Simiyu.
Jafo ameonyesha kufahishwa huko akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.
“Hamjamaliza kwa asilimia 100 ujenzi wa hospitali yenu lakini nimeridhika sana kwa kazi nzuri ya majengo yenu,” amesema Jafo.
Jafo amewataka viongozi na watendaji wa wilaya hiyo kukamilisha ujenzi huo ifikapo Julai 30 mwaka huu.
Katika Ziara hiyo, Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Itilima
Njalu Silanga kwa kuwapigania wananchi wake katika masuala mbalimbali
ya kimaendeleo.
Aidha,Njalu ameishukuru sana serikali kwa fedha Sh.Bilioni 1.5
zinazofanikisha ujenzi wa hospitali hiyo sambamba na fedha nyingi za
miradi mingine ya maendeleo ikiwemo fedha za ujenzi wa jengo la Utawala.
No comments:
Post a Comment