Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpokea Bw. Damas Shaltiel ambaye ni
Katibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe aliyekihama Chama cha
ACT Wazalendo na kujiunga na CCM baada ya Waziri Mkuu kuhutubia
Kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwenye
uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kadi ya ACT Wazalendo ya Bw.
Damas Shaltiel (kushoto) ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini,
Zitto Kabwe baada ya katibu huyo kukihama chama hicho na kujiunga na CCM
baada ya Mheshimiwa Majaliwa kuhutubia Kongamano lililoandaliwa na
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
mjini Kigoma, Julai 13, 2019.Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Gaudencia
Kabaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya CCM, Bw. Damas Shaltiel
ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe
aliyekihama Chama cha ACT Wazalendo na kujiunga na CCM baada ya Waziri
Mkuu kuhutubia Kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment