CCM DODOMA YAJIPANGA KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,MBUNGE MAVUNDE AMWAGA VIFAA VYA UCHAGUZI
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Dodoma
Mjini kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa 2019 kwa kuwafikia na kutatua kero,matatizo na
changamoto zinazowakabili wananchi wake na pia kuwasimamia Viongozi wote
wachaguliwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM na kutatua
matatizo ya wananchi.
Hayo yamesemwa leo katika Ukumbi wa White
House CCM Dodoma na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg Robert Mwinje wakati
wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya uenezi(Spika) na bendera kwa kata
zote 41 vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony
Mavunde kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Tunataka viongozi wote mliopo Serikalini
na wawakikishi wa wananchi mnaotokana na CCM kuhakikisha mnatatua
matatizo ya wananchi kuanzia ngazi ya chini kabisa ili tutengeneze
uhalali kwa wananchi kuja kuwaomba ridhaa mwaka huu 2019 na mwakani
2020″Alisema Mwinje
Akitoa maelezo ya awali,Mbunge wa Jimbo
la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amesema kwamba vifaa hivyo alivyotoa
leo kwa kila kata na Uongozi wa Wilaya wa Jumuiya Speaker 45 zenye
thamani ya Tsh 16,000,000 na bendera 1000 zenye thamani ya Tsh 3,500,000
ni maandalizi ya kampeni ya kisayansi ambayo wamepanga kuifanya katika
Jimbo la Dodoma ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika
uchaguzi huu wa serikali za Mitaa.
“Kupendeza kwetu kwa mashati ya kijani na
kuimba kwetu vizuri nyimbo za CCM hakuna maana kama hatutakua Chama cha
kujibu kero za wananchi.Nimejipanga vizuri kuhakikisha naendelea
kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuhakikisha Jimbo la Dodoma Mjini
linaendelea kutoa kura nyingi kwa CCM katika uchaguzi wa Rais,Wabunge
na Madiwani mwaka 2020.Rais Magufuli na CCM imetufanyia mambo makubwa
sana hapa Dodoma hususani Jimbo la Dodoma Mjini shukrani yetu tutailipa
kwenye sanduku la kura”Alisema Mavunde
Wakati huo huo,Mbunge Mavunde ameahidi
kutoka Tsh 20,500,000 kwa mgawanyo wa Tsh 500,000 kwa kata zote 41
katika kutunisha mfuko wa Uchaguzi wa Kata.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi wa
Chama Wilaya na Viongozi wa Chama na Jumuiya zote kwa ngazi ya kata zote
kwa Jimbo la Dodoma Mjini pamoja na Madiwani wa Kata na Viti Maalum.
No comments:
Post a Comment