Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza wakati alipotembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale
(Zinjanthropus Boisei), uliliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro,
Julai 22.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Khamis Kigwangala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akisalimiana na Balozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson, baada
kutembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei),
uliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa
ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo
alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde
la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya
miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale
(Zinjanthropus Boisei). Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Khamis Kigwangala na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa
ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo
alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde
la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya
miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus Boisei. Tokea
kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala, Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa,
Profesa Audax Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*******************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isimamie
uboreshaji wa eneo la mnara wa Zinjathropus ili paweze kuvutia zaidi.
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Julai 22, 2019) wakati akizungumza na
wananchi na viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi
ya ugunduzi wa fuvu la Zinjathropus Bosei, eneo la bonde la Olduvai, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.
Maadhimisho hayo yamefanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na uzinduzi wa makumbusho ya Dkt. Mary Leakey. Mnara wa Zinjathropus na Homo habilis umejengwa kwenye hifadhi ya Ngorongoro karibu na njia panda ya kuelekea bonde la Olduvai.
“Kwenye mnara wa Zinjathropus na Homo habilis pasiachwe
kama palivyo. Pajengwe seng’eng’e kuzunguka eneo lile lakini pia paweke
kibanda cha mlinzi ambaye pia atakuwa anatoa taarifa kwa wageni
wanaopita hapo.”
“Mtafute
vijana kadhaa ambao ni wenyeji wa eneo hili, wafundishwe historia
kamili kisha wapewe ajira hizo. Kibanda kikijengwa kwa juu kiwe na vioo
ili anayelinda aweze kuona pande zote na pia muweze kumkinga na vumbi na
upepo mkali wa eneo lile.”
Waziri Mkuu pia alitembelea korongo la Frida Leakey, (mahali ambapo zinjathropous aligunduliwa) na kupata maelezo juu ya kugunduliwa kwa fuvu la mtu wa kale duniani yapata miaka milioni mbili iliyopita.
Akigusia
kuhusu uhifadhi wa eneo hilo, Waziri Mkuu alisema nako pia pajengwe
kibanda cha mlinzi mwenye uwezo wa kutoa taarifa kwa watalii na
akasisitiza pia ajira hizo ziwahusu wenyeji wa eneo hilo.
“Kwenye
korongo la Frida, pawekwe bango lenye maelezo ya Kiswahili, nako pia
wapatikane vijana sita au nane, waeleweshwe hiyo historia, wakifuzu,
Wizara iwawezeshe, wapangiane zamu ya kushinda hapo. Pia pajengwe
kibanda cha wageni kupumzikia wakifika eneo hilo.
Kuhusu
makumbusho ya Dkt. Leakey, Waziri Mkuu alisema makumbusho hayo ni lulu
kwa Taifa. “Ninawapongeza viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Ngorongoro
kwa kuendeleza na kutunza makumbusho haya.”
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah
alisema kwa sasa dunia inatambua kuwa chimbuko la binadamu ni Afrika.
“Hata kama tunatofautiana sura na rangi, watu wote duniani wana asili ya
Afrika. “Kwetu sisi Tanzania, tunaadhimisha uvumbuzi huu kwa sababu
fuvu la Zinjanthropus ni alama na nembo ya Tanzania na dunia.”
Alisema maadhimisho hayo yataendelea kwa kufanya maonesho ya fuvu la Zinjanthropus boisei na malikale zingine katika mikoa sita ya Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Mtwara na Dodoma.
Alisema
wizara yake imebaini fursa zilizopo kwenye sekta ya urithi wa utamaduni
yaani malikale au utamaduni tuli (static cultural heritage) na
utamaduni hai (dynamic culture) ili kuvutia watilii na hivyo kuongeza
idadi yao na kuwafanya waongeze muda wa kukaa nchini (length of stay) na
hatimaye kuongeza pato la Taifa litokanalo na utalii.
“Wizara
yangu imeanza kuiboresha na kuendeleza sekta ya malikale na urithi wa
utamaduni ili izalishe mazao ya utalii na kuvutia watalii kwa kuhamisha
vituo vya Idara ya Mambo ya Kale na kuvipeleka TANAPA, TAWA, NCAA, TFS
na Makumbusho ya Taifa ili viendelezwe na kuwa vivutio vya utalii.
“Pia
tumehamishia Makumbusho ya Taifa kazi zote za uhifadhi wa urithi wa
utamaduni tuli au malikale na kuanzisha tamasha la urithi wa utamaduni
wa Mtanzania (Urithi Festival: Celebrating Our Heritage). Tamasha hili
litasherehekewa Septemba, kila mwaka.
Naye Balozi wa Marekani hapa nchini, Dk. Inmi Patterson ameipongeza Serikali kwa kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni.
Pia
alisifu utajiri wa rasilmali misitu na wa nyama ambao Tanzania
imejaliwa kuwa nao. “Uamuzi wa Rais Magufuli wa kuanzisha hifadhi ya
Burigi, unazidi kunogesha sifa ya Tanzania katika suala la hifadhi za
maliasili na utalii na katika kukuza urithi na utajiri wa nchi,” alisema
kwa Kiswahili fasaha.
Alisema
maadhimisho hayo ni siku muhimu kwake kwani yamewakutanisha watu wa
kaliba tofauti wakiwemo wanasiasa, wanasayansi, maprofesa kutoka
Uingereza, Marekani na Ujerumani, wanafunzi kutoka shule za Tanzania na
wenyeji wa Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment